WAZEE ZAIDI YA 500 KUPEWA ELIMU YA UJASIRIAMALI ARUSHA
Na Mery Kitosio, Arusha
ZAIDI ya wazee 500 kutoka katika kata za Sombetini,Elerai,na
Sokoni one Jijini Arusha wanatarajiwa kunufaika na elimu ya ujasiamali kutoka
katika shirika binafsi la Inform Sector
Team (INSET) ambapo wazee hao wataweza kuanzisha miradi mbalimbali ndani ya jamii zao na kuachana na tabia ya
kuwa tegemezi wa kila kitu.
Akiongea na “Jambo leo’
mjini hapa mapema jana mara baada ya kuwapa semina hiyo baadhi ya wazee wa kata hizo tatu Mkurugenzi mtendaji wa
Shirika hilo Japhet Sauni alisema kuwa mpango huo tayari umeshaanza kutekelezwa
kwa baadhi ya wazee na lengo halisi ni
kuachana na umaskini ambao unasababisha
Umaskini mkubwa
Japhet alisema kuwa shirika hilo
limeamua kufikia uamuzi huo mara baada ya kuona kuwa asilimia kubwa sana ya wazee wanapata shida ndani ya jamii zao kwa kuwa
hawana vipato vya kutosha huku hali hiyo ikisababisha baadhi yao kufa kabla ya wakati na kuacha familia
zao zikiwa Yatima.
Aliongeza kuwa Uamuzi huo wa shirika hilo
la kuwapa wazee hao 500 elimu ya ujasiamali utaweza kuwasaidia kubuni biashara
mbalimbali ambazo zitaweza kuwanufaisha na kuwafanya waweze kujimudu katika
maisha yao ya
kila siku sanjari na kuweza kujihudumia katika maitaji ya msingi ambayo
yanakosekana katika familia zao.
“leo unakuta mzee anakaa tu nyumbani anasubiri kuomba omba
na kupewa vyakula na watoto wao lakini pindi hawa watoto wanapokosa riziki hawa
wazee wanaaza kuandamwa na magonjwa kwa kuwa hawana hata vyakula lakini kama wakianza kuwa
wajasiamali wa biashara ndogondogo basi watachangia sana kuondokana na umaskini
ambao umekithiri sana kwenye maisha ya baadhi ya wazee wa leo kwa kuwa baadhi yao bado wanaonekana kuwa na
nguvu kubwa ya kuweza kuendeleza biashara mbalimbali lakini bado hawana elimuy
ya kutosha ’aliongeza.
Pia alisema kuwa mara baada ya wazee hoa kuweza kupatiwa
elimu ya ujasimali ambayo imeanza kutolewa kwa wazee hao kuanzia sasa wataweza
kuanzisha miradi mbalimbali ambapo kupitia miradi hiyo wataweza kujiunga na Chama cha kuweka na kukopa cha wazee hali ambayo nayo
itaweza kuboresha sana
maisha ya wazee hasa wa Jiji la Arusha.
‘tunachokiitaji hapa ni wazeee hawa wainuke na waachane na
tabia ya kuwa tegemezi zaidi,na kama wakishapata elimu hii ya ujasiamali bado
shirika halitaweza kuwaacha badala yake tunawapa mbinu mbalimbali za kuboresha
miradi baada ya hapo sasa tunawapeleka katika Saccos ya wazee na mpaka kufika
hapo tunakuwa tumewasaidia wazee hawa kwa kiwango cha hali ya juun sana tofauti
na pale kama tungewaacha kwenye jamii zao’aliongeza Japheti.
Alimalizia kwa kusema kuwa wazee wa Kitanzania hawapaswi
kukata tama ya maisha kwa kuwa wana umri
mkubwa sana badala yake wanatakiwa muda ambao
wanakaa majumbani mwao kuweza kuutumia kiujasimali ambapo kama watafanya hivyo
basi watachangia sana
hata baadhi ya Vijana nao kuweza kuimarisha uchumi wao wa kila siku.
MWISHO
No comments:
Post a Comment