SEIKALI imetakiwa kuzipa ruzuku kubwa shule za
pembezoni ili kuwezesha shule hizo kupata vitendea kazi vya masomo na miundo
mbinu bora yatakayoweka mazingira sawa ya ushindani kitaaluma
katika mitihani ya kitaifa.
Shule nyingi za pembezoni zinadaiwa kukosa mabweni
,madarasa ,maabara na waalimu wa kutosha hali inayowanyima wanafunzi walio
wengi wanaosoma katika shule hizo kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao
ya kitaifa.
Akihutubia wananchi katika mahafali ya kidato cha nne
katika shule ya Sekondari ya Soit Sambu Wilayani Ngorongoro mratibu wa shirika
la misaada la Focus
On Tanzanian Communities Happy
Mwamasika alisema mazingira ya shule za vijijijini ni mabaya na magumu.
“Ni wazi sote leo tunajionea mazingira ya shule hii
,haina hata maabara ya somo la sayansi na watoto wanafundishwa
masomo hayo hapa watawezaje kufanya mitihani ya masomo hayo na kufaulu kama
wengine wa mijini”alihoji Mwamasika.
Alisema kuwa ni lazima kuwepo kwa mazingira ya haki
ili kuondoa matabaka na ubaguzi katoka mfumo wa Taifa wa elimu.
Alisema kuwa shirika hilo litajenga bweni la kisasa
litalaoweza kuchukua wanafunzi zaidi ya mia moja na kupunguza msongamno katika
bweni moja lililopo ambalo wanafunzi watatu wanalala katika kitanda kimoja.
“Nimetishwa na mazingira niliyoyaona bweni lillopo
linapaswa kuchukau wanafunzi themanini lakini wanalala watoto zaidi ya mia
mbili hali hii inatisha”alisema Mwamasika.
Aliwataka wananchi wa eneo hilo na wazazi wa wanafunzi
kuchangia maendeleo ya shule hiyo na kuwato wasiwasi kwa kuiwa wajumbe wote wa
bodi ya wakurugenzi ya FOTZC wanatambua umuhimu wa elimu kwa mtoto wa
kike na kwamba hilo litajengwa hivi karibuni.
Aidha alitambua mchango wa kampuni ya kitalii ya
Thomson kwa kulipa shirika hilo fursa ya kutangaza ashughuli na kupata michango
kutoka kwa wahisani mbalimbali wa miradi ya kijamii.
“Naishukuru kampuni hii kipekee wasingetupa
fursa ya kutangaza kazi zetu kupitia makambi yao, leo hii tusingeweza kuwa na
nyumba za walimu katika shule hii wala tusingekuwa katika mchakato wa kujenga
bweni la wasichana tutakalolijenga mwishoni mwa mwaka huu”alisema Mwamasika.
Alisema kuwa kampuni ya Thomson ni mfano tu wa namna
ya kuonyesha ni kwa jinsi gani jamii zinaweza kunufaika na utalii
endapo utafanywa kwa dhamira ya kuendeleza jamii na bila upotoshwaji.
No comments:
Post a Comment