Na Queen Lema, Arusha
NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA ILI KUEPUKANA NA HASARA MBALIMBALI
Nchi za Afrika zimetakiwa kuhakikisha kuwa zinajiwekea
utaratibu wa kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vya hali ya juu sana ili kuweza kujiepusha
na hasara zinazotokea kwenye ukaguzi, pamoja na kwenye masoko mbalimbali ya
uuzaji wa bidhaa hizo.
Hayo yameelezwa mjini hapa na kaimu mkurugenzi mkuu shirika
la viwango Tanzania(TBS)Bw Leandri Kinabo wakati wa mkutano wa baraza la utendaji la mashirika ya viwango Afrika
linaloshirikisha nchi 11 (ARSO)unaendelea mjini hapa
Bw Kinabo alisema kuwa nchi za Afrika zinatakiwa kuhakikisha
kuwa zinakuwa marafiki wazuri wa kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vya
hali ya juu sana kwani uzalishaji wa bidhaa ambazo hazina ubora ni chanzo
kikubwa sana cha hasara hasa kwa wenye viwanda na kwa watumiaji wenyewe.
Alifafanua kuwa bidhaa zenye ubora zinachangia sana maendeleo ya Nchi na
Bara jambo ambalo kila mdau anatakiwa kuhakikisha kuwa anafuata taratibu na
sheria za uzalishaji bora ili kuweza kuraisisha hata biashara zao tofauti na
pale ambapo bidhaa zinakosa ubora ambao unaitajika
“kama nchi za bara la afrika na Tanzania itaweza kuzalisha
bidhaa zenye ubora ni wazi kuwa wataweza kuchochea sana maendeleo kwa kuwa hata
biashara nazo zitaweza kukua na kuimarika zaidi kwenye ubora wa hali ya juu
lakini kama watakuwa wanakwepa njia mbalimbali za uzalishaji bora basi
watachangia sana umaskini hasa wan chi hizi ingawaje kuna rasilimali nyingi
sana”aliongeza bw Kinabo
Katika hatua nyingine alifafanua kuwa ili kuboresha zoezi hilo la ubora wa bidhaa
hasa kwa nchi za Afrika wataweza kujadili masuala mbalimbali ambayo yataweza
kufanya nchi zote kutumia kiwango kimoja cha ubora tofauti na pale ambapo kila
nchi inapotumia viwango vyake vya ubora.
Alisema kuwa kupitia utaratibu huo wa kutumia viwango
vinavyofanana kwa nchi zote za Afrika
wadau mbalimbali hususan wafanyabiashara wataweza kuepukana na vikwazo
mbalimbali ambavyo vinachangia sana kukwamisha
malengo yao
mbalimbali kutokana na Ubora wa bidhaa kwa nchi husika
“ndani ya baraza hili tutaweza kuweka utaratibu maalumu wa
kuhakikisha kuwa tunatumia viwango ambavyo vinafanana na hii itasaidia sana
kuweza kuharakisha maendeleo kwa bidhaa na biashara mbalimbali tofauti na pale
ambapo kila nchi inakuwa na utaratibu wake wa viwango lakini njia hii ni raisi
sana hivyo tutawekeana mikakati mbalimbali ya kuhakikisha hilo
linaboreshwa”aliongeza bw Kinabo
Alimalizia kwa kusema kuwa nao wananchi wa Tanzania
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajiwekea utaratibu wa kutumia na kuimarisha
zaidi bidhaa ambazo zina ubora wa hali ya juu kwani kwa kutotumia bidha ambazo
hazina nembo ya shirika la viwango nchini pamoja na ubora unaoitajika na Serikali ni
chanzo cha madhara makubwa sana kwa watumiaji wa bidhaa
No comments:
Post a Comment