RAIS KAGAME ADAI ICC IMEAANZISHWA KWA AJILI YA WAAFRIKA
Na Hirondelle,Arusha
Arusha,
Oktoba 05, 2012 (FH) – Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Alhamisi amedai
kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) yenye mamlaka ya
kuwashitaki watuhumiwa wa mauaji ya kimbari,uhalifu wa kivita na uhalifu
dhidi ya binadamu, ni fimbo ya kisiasa iliyoanzishwa kwa lengo la
kuwapiga waafrika.
‘’Wanaiita
mahakama ya kimataifa lakini kwa kweli ni kwa ajili ya waafrika.
Waafrika siyo lazima wale ambao wamefanya makosa, bali ni wale
wanaowapinga,’’ Rais Kagame alisema mjini Kigali wakati akizindua Mwaka
wa Mhakama wa 2012-2013 nchini humo.
Rais
huyo alifafanua ’’ Wanatuambia, ooh watawaadhibu watu wanaojihusisha
katika kusajili askari watoto lakini hawawasaki wale wanaowaua.’’
Kagame
aliendelea ‘’Wapo watu wanaoua,wanaobaka na wanaofanya kila
uhalifu.Hunyamaza tu juu ya hayo yote labda ni kwa sababu tu ndivyo
waafrika wanavyotakiwa kuwa.’’
Rais
huyo pia alizungumzia mgogoro unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) akidai kwamba serikali ya nchi hiyo na jumuia
ya kimataifa ndiyo inayostahili kushutumiwa na siyo Rwanda.
Baadhi
ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) yameiomba Rwanda kuunga mkono
juhudi za kumtia mbaroni Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye anatakiwa na
ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.Lakini Rais
Kagame amekuwa wakati wote akidai kwamba nchi yake haina sababu yoyote
ya kufanya hivyo.
NI/FK
No comments:
Post a Comment