Na Queen Lema, MERU
IMEELEZWA kuwa kutokana na uhaba wa maji katika shule ya
Sekondari Malula iliopo Wilayani Meru mkoani Arusha zaidi ya wanafunzi ishirini
kwa kila siku wanashindwa kuhudhuria masomo kwa kuhofia kutembea umbali wa
kilomita zaidi ya nne kwa ajili ya kutafuta maji
Akiongea na waandishi wa habari jana mkuu wa shule hiyo Bi
Rehema Mroso alisema kuwa changamoto hali hiyo imedumu kwa miaka minne sasa
Bi Rehema alisema kuwa hali hiyo imekuwa ni kero kubwa sana kw wanafunzi wa shule hiyo kwani mara nyingine
imekuwa ikisababisha wanafunzi kutumia muda mwingi sana kufikiria zaidi maji kuliko masomo ya
kila siku.
Alifafanua kuwa wanafunzi hao wanalazimika hata kutembea
umbali wa kilomita zaidi ya nne ili kutafuta maji wakati wa muda wa masomo hali
ambayo ni chanzo kikubwa sana
cha utoro wa wanafunzi shuleni hapo.
“kwa kweli wanafunzi kwa sasa wapo katika hali mbaya sana
kwa kuwa wanshindwa kuwaza masomo na wanawaza umbali mrefu sana ambao
wanatembea ili kutafuta maji ambapo ni kutoka hapa hadi katika uwanja wa ndege
wa Kilimanjaro sasa hali hii kama haitaweza kudhibitiwa kwa haraka sana basi
itachangia sana wanafunzi kukumbwa na mdororo wa elimu hasa katika maeneo haya
ya Kingori, na Malula”aliongeza Bi Rehema.
Pia alisema mbali na kukabiliwa na changamoto wanafunzi
kushindwa kuhudhuria masomo kutokana na kuhofia kubeba maji umbali mrefu pia
shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi
hali ambayo imeifanya shule hiyo kuweza kuajiri walimu ambao ni wanafunzi ili
kuweza kuwasadia wanafunzi hao
Bi Rehema alisema kuwa wamelazimika kuajiri walimu wawili
ambao ni wahitimu wa kidato cha sita waweze kuwafundisha wanafunzi hao masomo
hasa ya Sayansi hali ambayo bado nayo ni changamoto kubwa sana
ya wanafunzi kushindwa kufanya vema zaidi katika masomo yao
hasa masomo ya hesabu na phizikia ambayo ndiyo kipaumbele kikubwa sana cha Serikali kwa
sasa.
‘sasa hivi Serikali inakazia sana masomo ya Sayansi yaweze
kupewa kipaumbele lakini kitu cha kushangaza ni kuwa hapa kwetu hatuna kabisa
walimu na hawa walimu tulionao ni wanafunzi tu tena wa kidato cha sita sasa
hili nalo linachangia sana kuweza kuwafanya wanafunzi wengi kukata tamaa na kushindwa
kuyapa haya masomo kipaumbele kikubwa kama ilivyo kwa shule nyingine hasa
kwenye masomo hayo”aliongeza Bi Rehema.
Alimalizia kwa kusema kuwa Serikali inatakiwa kutatua kwa
haraka sana kero ambazo zinaikabili shule hiyo kwa kuwa shule hiyo ni moja ya
shule ambayo inatumiwa na wakazi wengi hasa wa mpaka wa wilaya ya Meru na mkoa
wa Kilimanjaro
MWISHO
No comments:
Post a Comment