Friday, October 19, 2012

CHAMA CHA UNUNUIZ NA WAGAVI CHAJIPANGA KUKABILIANA NA TATIZO

NA GLADNESS MUSHI, ARUSHA

CHAMA cha ununuzi na wagavi Tanzania kimejipanga kukabiliana na tatizo la rushwa ambalo limekuwa likipelekea miradi mingi kuwa chini ya viwango na kupelekea fedha za serikali kupotea bila kuwa na faida kwa wananchi husika.

Hayo yamesemwa mwenyekiti wa chama cha  wanunuzi na wagavi nchinin kenya( KISIM) bw.Injini Chris Oanda  wakati akizungumza katika kongamano la kwanza  la chama hicho linaloendelea mjini hapa.

Ijinia Oanda alisema kuwa swala la rushwa limekuwa ni changamoto kubwa sana katika jamii zetu hali ambayo inapelekea miradi mingi ya serikali kama barabara kuwa chini ya kiwango kutokana na rushwa hivyo ni kongamano hilo litawawezesha kujadili kwa kina na kutafuta mbinu madhubuti za kutatua changamoato hiyo.

Aidha alifafanua kuwa mpango wa ununuzi unaunganisha watu wengi zaidi hivyo ni lazima kuwe na namna ya kuzuia rushwa kwa kuwa wanaolaumiwa ni wasimamizi hivyo ni lazima wajisafishe kwa kutokupokea rushwa.

 Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho nchini Tanzania (PASAT) bw.Nolaskus Mpota alisema kuwa lengo la kukutana ni kujadili changamoto kubwa ya kuhusiana na viwango katika ununuzi na ugavi kwamba wamegundua kuwa miradi mingi kutokuwa na viwango vya uhakika.

Bw.Mpota alisema kuwa ni lazima kuwe na viwango na mtu atakuwa anajua matokeo ya kazi ambayo inafanywa hata kabla ya kazi haijaanza  ili iwe rahisi kwa mgavi ama mnunuzi kumchukulia hatua toka mwanzo au kufanya marekebisho mapema.

Alifafanua kuwa miradi kujengwa  chini ya kiwango wengi wa wazabuni hapa nchini hawafuatilia vigezo wala hawasomi vizuri makabrasha na kujituma kwa kuwa ununuzi ni utandawazi hivyo bila kujituma ndio kila kitu ikiwa ni pamoja na kuzingatia vigezo.

No comments:

Post a Comment