BI VICKY AMBAYE NI MENEJA WA BENKI YA NMB KWA KANDA YA KASKAZINI AKIPOKEA CHETI KAMA ISHARA YA USHINDI KATIKA MAONESHO YA NANENA NE AMBAPO MGENI RASMI ALIKUWA NI MIZENGO PINDA
NMB YAHIDI KUBORESHA KILIMO CHA WAKULIMA WADOGO WADOGO KWA
KANDA YA KASKAZINI
BENKI ya NMB kanda ya
kaskazini imesema kuwa ina mikakati mbalimbali ya kuweza kuimarisha kilimo hasa
kwa wakulima wadogo wadogo sanjari na kutoa mikopo mbalimbali kama
vile Pembejeo kwa wakulima hao wadogo wadogo ili kufanya Kilimo chao kuwa cha
Kisasa zaidi
Hayo yameelezwa na Bw Ally Jamali ambaye ni afisa uhusiano
kilimo katika benki hiyo wakati alipokuwa akiongea na Waziri Mkuu Bw Mizengo
Pinda ambaye alitembelea banda la NMB katika viwanja vya Nane nane (TASO)mapema juzi
Aidha bw Jamali alisema kuwa ili kumkomboa Mkulima wa sasa
Benki hiyo imejidhatiti kuhakikisha kuwa
wakulima wadogo wadogo wanapata huduma za msingi ili nao waweze kufikia
malengo yao
mbalimbali ambayo wamejiwekea
Alifafanua kuwa kwa sasa kupitia mfum wa Stakabadhi ya mazao
ghalani (WRS) wwakulima wa kanda ya kaskazini wameweza kupata mikopo ya aina
mbalimbali ambapo lengo ni kukomboa zaidi Kilimo kwanza
“huu mfumo na mingine inayokuja itaweza kusaidia sana
kushamiri na kustawi kwa mazao mbalimbali ambayo yana tegemewa ndani ya kanda
yetu ambapo kwa sasa tuna mazao kama vile Kahawa,Mbaazi, Mahindi, pamoja na
Korosho huku mpaka sasa matunda na mafanikio mbalimbali yameshaonekana kupitia
mfumo huu”aliongeza Bw Jamali.
Pia alisema kuwa ili kuendelea kuboresha zaidi hali ya
Kilimo wamefanikiwa kufanya majaribio ya pembejeo kwa ajili ya wakulima wa
mbogamboga ambapo Kama zoezi hilo nalo
litakamilika basi litachangia sana
kukuza na kuimarisha hata uchumi wa wakulima hao.
Aliongeza kuwa Pembejeo hizo za wakulima wadogo wadogo
zitakuwa na faida kubwa sana kwenye kilimo chao
kwani hapo awali wakulima hao walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
hali ambayo ilifanya washindwe hata kukopesheka na Taasisi mbalimbali za Fedha
nchini lakini kupitia Pembejeo hizo wataweza kuzalisha kwa nguvu kubwa hivyo
kukopesheka kwa Uraisi sana.
“kwa hapo awali wakulima hawa ambao ni wadogo wadogo
walikuwa wanashindwa kuaminika kwa uraisi sana lakini kama watafanikiwa
kuuungana nasi katika mikopo na mazoezi kama haya watachangia kwa kiwango
kikubwa kubadilisha hata aina ya kilimo ambacho wanalima kwa sasa na kuwa
kilimo cha kisasa zaidi”aliongeza bw Jamali
Katika hatua nyingine aliwataka wakulima hasa wadogo wadogo
kuhakikisha kuwa wanaachana na dhana ya kuogopa Taasisi mbalimbali za fedha na
kuhakikisha kuwa wanafuatilia kwa ukaribu kwani hata wao wana nafasi kubwa sana ya kuweza kukopa na
kufikia ndoto zao mbali mbali ambazo wanazo katika kilimo
No comments:
Post a Comment