Sunday, September 22, 2013

WAZIRI NAGU ATAKA MCHANGO WA WALIMU KWENYE TAIFA LA TANZANIA UJULIKANE

dkt Mary Nagu

Serikali imetakiwa kuhakikisha kuwa inatambua na kuthamini zaidi kazi za walimu hapa nchini lakini pia kuwajengea mazingira mazuri ya kazi kwani kama watabaguliwa na kisha kuachwa nyuma ni wazi kuwa sumu mbaya itatembea kwenye maisha ya wanafunzi

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dkt Mary Nagu katika maafali ya nne ya shule ya Msingi haradali iliopo Wilayani Meru mkoani Arusha mapema leo.

Dkt Nagu alisema kuwa Serikali lakini hata nao wanachi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawajengea walimu mazingira mazuri ya kufanya kazi kwani wao wanamchango mkubwa sana kwenye taifa

Alisema kuwa kama wadau mbalimbali lakini pia Serikali itafanya hivyo ni wazi kuwa walimu watafundisha kwa moyo bila kujali aina ya shule na changamoto ambazo wanakabiliana nazo mabazo wakati mwingine ndio chanzo kikubwa cha mdondoko wa elimu

Alifafanua kuwa kama walimu wa nchi ya Tanzania watakuwa wanafanya kazi bila kupewa kipaumbele cha hali ya juu sana basi wao watakuwa mabalozi wazuri wa kupandikiza mbegu mbaya kwa wanafunzi na hatimaye madhara yatajionesha muda usio mrefu.


Wakati huo huo mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo ya Haradani,Bw Simon Kaaya
alisema kuwa ili kukuza na kuwekeza kwenye sekta hiyo ya elimu hapa nchini Changamoto mbalimbali zinatakiwa kutatuliwa kwa haraka sana kwani bado kuna umuhimu mkubwa wa elimu.

Bw Kaaya alisema kuwa mbali na hayo hata wamiliki wa shule mbalimbali wanatakiwa kuangalia zaidi suala la mahitaji kuliko suala la maslahi ambalo wakati mwingine linasababisha baadhi ya watoto kukosa elimu kabisa.



No comments:

Post a Comment