Saturday, August 11, 2012

NMB YAAHIDI KUWASAIDIA WAKULIMA WADOGO WADOGO

BI VICKY AMBAYE NI MENEJA WA BENKI YA NMB KWA KANDA YA KASKAZINI AKIPOKEA CHETI KAMA ISHARA YA USHINDI KATIKA MAONESHO YA NANENA NE AMBAPO MGENI RASMI ALIKUWA NI MIZENGO PINDA





NMB YAHIDI KUBORESHA KILIMO CHA WAKULIMA WADOGO WADOGO KWA KANDA YA KASKAZINI

BENKI ya NMB  kanda ya kaskazini imesema kuwa ina mikakati mbalimbali ya kuweza kuimarisha kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo sanjari na kutoa mikopo mbalimbali kama vile Pembejeo kwa wakulima hao wadogo wadogo ili kufanya Kilimo chao kuwa cha Kisasa zaidi


Hayo yameelezwa na Bw Ally Jamali ambaye ni afisa uhusiano kilimo katika benki hiyo wakati alipokuwa akiongea na Waziri Mkuu Bw Mizengo Pinda ambaye alitembelea banda la NMB katika viwanja vya Nane nane (TASO)mapema juzi

Aidha bw Jamali alisema kuwa ili kumkomboa Mkulima wa sasa Benki hiyo imejidhatiti kuhakikisha kuwa  wakulima wadogo wadogo wanapata huduma za msingi ili nao waweze kufikia malengo yao mbalimbali ambayo wamejiwekea

Alifafanua kuwa kwa sasa kupitia mfum wa Stakabadhi ya mazao ghalani (WRS) wwakulima wa kanda ya kaskazini wameweza kupata mikopo ya aina mbalimbali ambapo lengo ni kukomboa zaidi Kilimo kwanza

“huu mfumo na mingine inayokuja itaweza kusaidia sana kushamiri na kustawi kwa mazao mbalimbali ambayo yana tegemewa ndani ya kanda yetu ambapo kwa sasa tuna mazao kama vile Kahawa,Mbaazi, Mahindi, pamoja na Korosho huku mpaka sasa matunda na mafanikio mbalimbali yameshaonekana kupitia mfumo huu”aliongeza Bw Jamali.

Pia alisema kuwa ili kuendelea kuboresha zaidi hali ya Kilimo wamefanikiwa kufanya majaribio ya pembejeo kwa ajili ya wakulima wa mbogamboga ambapo Kama zoezi hilo nalo litakamilika basi litachangia sana kukuza na kuimarisha hata uchumi wa wakulima hao.

Aliongeza kuwa Pembejeo hizo za wakulima wadogo wadogo zitakuwa na faida kubwa sana kwenye kilimo chao kwani hapo awali wakulima hao walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hali ambayo ilifanya washindwe hata kukopesheka na Taasisi mbalimbali za Fedha nchini lakini kupitia Pembejeo hizo wataweza kuzalisha kwa nguvu kubwa hivyo kukopesheka kwa Uraisi sana.

“kwa hapo awali wakulima hawa ambao ni wadogo wadogo walikuwa wanashindwa kuaminika kwa uraisi sana lakini kama watafanikiwa kuuungana nasi katika mikopo na mazoezi kama haya watachangia kwa kiwango kikubwa kubadilisha hata aina ya kilimo ambacho wanalima kwa sasa na kuwa kilimo cha kisasa zaidi”aliongeza bw Jamali

Katika hatua nyingine aliwataka wakulima hasa wadogo wadogo kuhakikisha kuwa wanaachana na dhana ya kuogopa Taasisi mbalimbali za fedha na kuhakikisha kuwa wanafuatilia kwa ukaribu kwani hata wao wana nafasi kubwa sana ya kuweza kukopa na kufikia ndoto zao mbali mbali ambazo wanazo katika kilimo

No comments:

Post a Comment