Monday, October 29, 2012

RAISI JAKAYA KIKWETE KUZINDUA CHUO CHA NELSON MANDELA NOVEMBER 2

RAISI JAKAYA KIKWETE



RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kufungua chuo kikuuu cha Nelson Mandela
cha Sayansi na Teknolojia November 2 mwaka huu ambapo chuo hicho
kinatarajia kufanya mabadiliko mbalimbali kwa nchi ya Tanzania kufanya
  utafiti  katika maeneo  mbalimbali ya fani ya sayansi, uhandisi na
teknolojia.



Hayo yalisemwa jana na Makamu wa mkuu wa chuo hicho, Profesa Burton
Mwamila wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana
na maendeleo , mikakati ya chuo hicho kwa nchi ya Tanzania na mabara
mengine.



Alisema kuwa,  Rais Kikwete pamoja na wageni wengine kutoka nje ya
nchi wataweza kuhudhuria katika uzinduzi huo huku baadhi ya wageni hao
wakiweza kuona maendeleo pamoja na mikakati ya chuo hicho cha
kisayansi hali ambayo itaweza kutangaza vyema nchi ya Tanzania
kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma za kisayansi zilizopo  katika
jamii.



Alifafanua kuwa, mara baada ya viongozi hao kufungua rasmi chuo hicho
wataanza kuhakikisha kuwa chuo hicho kinakuwa na faida kwenye jamii
hali ambayo itaweza kupunguza na kuondoa matatizo mbalimbali hasa
kwenye fani za sayansi ,uandisi na teknolojia kwa ajili ya maendeleo
ya taifa na kuweza kupata wataalamun wenye uwezo na ujuzi  wa kutosha
.



‘Tunategemea mabadiliko makubwa sana hasa kwa nchi ya Tanzania kwani
chuo hiki kina uwezo mkubwa sana wa kuwapa fursa watanzania kuwa na
ujuzi wa kutosha hasa katika maswala ya tafiti na sayansi na kama
watanzania wataweza kukitumia vyema ni wazi kuwa fursa nyingi
zitaongezeka sana na ndio maana tumemwalika Rais Kikwete aweze
kufungua rasmi na viongozi wengine mbalimbali kutoka
ulimwenguni’alisema Profesa Mwamila.



Alisema kuwa, ili kujua kuwa chuo hicho kina nafasi kubwa sana kwa
watanzania chuo hicho kimeamua kudahili jumla ya wanafunzi 83 huku
wanafunzi 30 wanachukua masomo ya uzamivu na 53 ni mafunzo ya uzamili
ambapo kama wote hao watamaliza masomo ya vyema basi wataweza
kuchangia kuongezeka kwa pato la taifa na hatimaye uchumi wan chi
kukua.



Mwamila alisema kuwa, katika mwaka huu wa masomo chuo kimedahilin
wanafunzi 135 wa kundi la pili, huku kati yao 46 wanachukua masomo ya
uzamivu na 89 watachukua masomo ya uzamili huku asilimia 22 ni
wanawake , ambapo chuo hicho kwa sasa kina jumla ya wataalamu
watarajiwa 217 kati yao asilimia 20 ni wanawake.



‘Ili kujua kuwa masomo ya sayansi ni muhimu kwa wanawake tumehakikisha
kuwa idadi ya wanawake inakuwa kwa kasi tofauti na vyuo vingine nah ii
itasaidia kufanya taaluma ya sayansi kuwa na wataalamu wengi ambao ni
wanawake tofauti na ilivyo hivi sasa kuwa wenye taaluma wengi ni
wanaume,ingawaje kuna fursa kama ya chuo hicho lakini haitumiwi
ipasavyo ‘alisema Mwamila.



MWISHO