Wednesday, July 4, 2012

KANISA LA KKKT KIMANDOLU LAFANIKIWA KUNUNUA GARI JIPYA LENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 40

ASKOFU THOMAS LAIZER AKIWEKA WAKFU GARI LA KANISA KIMANDORU

  Askofu wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri tanzania
dayosisi ya kaskazini kati Dr Thomas Laizer akizindua rasmi gari la
usharika wa kimandolu uliopo mijini hapa ,mapema leo hii .
Gari ambalo lilizinduliwa rasmi  ambalo ni gari aina
ya Rord Renger  namba za usajili T 474 BRS lenye thamani ya
shilingi milioni 40 ambapo waumini wa usharika huo  walitoa michango
yao  kwa ajili ya kununua gari hilo ili limwezeshe mchungaji wa kanisa
hilo kufanya kazi yake kiufanisi.Picha na Queen Lema, Arusha

WAUMINI WANUNUA GARI AINA YA FORD RANGER LA ZAIDI YA MILIONI 40 KWA AJILI YA SHUGULI ZA INJILI


Askofu wa kanisa la KKKT dayosisi ya kaskazini Kati,Dkt Thomas Laizer ameyataka makanisa kujiwekea utaraibu wa kufanya maombi kila mara kwa kuwa sasataifa linapoteza rasilimali watu kutokana na migomo ambayo inaendelea kila mahala.

Dkt Laizer aliyasema hayo wakati wa ibada ya kuweka wakfu gari la kanisa la KKKT usharika wa Kimandolu mapema jumapili iliyopita jijini hapa.

Askofu huyo alifafanua kuwa kwa sasa Taifa la Tanzania lina ingia kwenye migogoro ya aina mbalimbali hali ambayo kama kanisa haitaliangalia kwa undani sana basi itaweza kupoteza mambo mengi

Alifafanua kuwa ni vema kuhakikisha kuwa kila mara maombi yanafanyika na kuliombea taifa kwa kuwa hiyo ni kazi mojawapo ya kanisa la leo na kanisa kama kanisa linanguvu kubwa sana ya kuweza kutetea jambo hilo

“leo madaktari wameingia kwenye migogoro na wamegoma lakini ukiangalia suala zima la vifo hasa kwa wanawake na watoto nalo linaongezeka sana sasa hali hii ni mbaya sana na kama hatutaomba rehema za Mungu juu ya nchi yetu basi hata kesho utasikia wengine nao wamegoma ingawaje kwa madaktari wanachokidai ni halali kabisa”alifafanua Dkt Laizer

Alisema kuwa ingawaje madaktari  hao wana haki ya kugoma lakini wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakumbuka kuwa na huruma ya Mungu kwa kuwa wanaokufa hawana hatia bali yenye hatia ni Serkali na kwa hali hiyo wanatakiwa hata kukumbuka amri za Mungu ambazo zinadai na kusema kuwa watu wanatakiwa kupendana.

Awali dkt Laizer aliongeza kuwa endapo kama kanisa litafanya maombi mbalimbali kwa taifa pia linatakiwa kuomba juu ya haki kwa kuwa kwa sasa kuna baadhi ya maeneo ambayo hayatoi haki kwa watanzania hali ambayo ndiyo chanzo kikubwa sana cha Rushwa.

“kwa sasa hivi rushwa imejaa kila mahali watu wananyimwa haki zao za msingi na hili limejitokeza hata kwenye uchaguzi wa EAC ambapo kulikuwa na rushwa nje nje na vyombo vy a usalama vilikuwa pale lakini hawaliangalia hilo na sisi kama tutaruhusu hilo ni wazi kuwa hata jamii zitakosa haki zao za msingi”aliongeza Dkt Laizer.

Katika hatua nyingine mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Bw Solomon Masangwa alisema kuwa mchakato wa kununua gari hilo  ulianza toka miezi michache iliyopita kutokana  na uitaji uliokuwepo

Bw Solomon alifafanua kuwa uitaji huo ulisababisha washarika waweze kuchanga zaidi ya Milioni 40 ili waweze kununua gari hilo ambalo wamenunua kwa ajili ya shuguli mbalimbali za kueneza injili.

Alizitaka sharika nyingine kuiga mfano kama huo ambapo waumini kama waumini wana uwezo mkubwa sana wa kununua vifaa maalumu kwa ajili ya kuendesha injili na kuacha kuwategema zaidi wafadhili.



No comments:

Post a Comment