Jamii kwa kushirikiana na viongozi mbali mbali wameombwa
kujitoa kwa hali na mali kumsaidia mjane aliyeunguliwa na nyumba yake
katika kitongoji cha kanisani kata ya Imbaseny katika halmashauri ya
Meru ili kumwezesha aweze kurudia katika hali yake ya kawaida.
Wito huo umetolewa na mhadhiri mwandamizi chuo kikuu cha
tumaini makumira ambae pia ni mjumbe wa mkutqno mkuu ccm taifa dr
danieli mirisho palangyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kukabidhi misaada ya mabati na mchele kwa mjane huyo
aliyeunguliwa na nyumba yake hivi karibuni katika kitongoji cha
imbaseny .
Dr Palangyo amesema kuwa kufuatia janga kubwa alilopata
mjane huyo ambae aliunguliwa na nyumba yake hivi karibuni kutokana na
chanzo ambacho hadi sasa hakijajulikana jamii,na viongozi mbali mbali
ndani ya wilaya ya arumeru wanapaswa kuungana kwa pamoja na jamaa
wanaojitolea kumsaidia mjane huyo ili aweze kujengewa nyumba yake na
kuweza kurudi katika hali yake kwani kwa sasa anaishi mazingira magumu
sana.
Amedai kuwa akiwa kama kiongozi amewiwa kufika kwa mjane
huyo na kuweza kutoa bati 23 pamoja na mchele kg 25 kwani mama huyo
pamoja na watoto wake wapo katika hali ngumu ambayo bila michango
hataweza kurejea katika hali yake.
Akizungumza mara baada ya kupokea kwa misaada hiyo mjane
huyo aliyetambulika kwa majina ya Maria Kimario mkazi wa imbaseny
alisema kuwa nyumba yake iliungua tarehe 29 mwezi uliopita na
kusababisha kupata hasara ya milioni 16 kwani vifaa vyote viliteketea
kwa moto huo huku chanzo cha awali kikiwa bado hakijajulikana kwani
alikuwa anatumia umeme unaotokana na Mobisol.
Aidha bi maria aliwaomba wadau mbali mbali kujitokeza na
kumsaidia ili aweze kurejea katika hali yake kwani kwa sasa anaishi
mazingira magumu pamoja na watoto wake huku akiwa hana chochote ikiwemo
nguo,chakula ,na mahala pa kuishi
No comments:
Post a Comment