Tuesday, February 28, 2012

KIJANA AELEZA JINSI ALIVYOMPACHIKA MAMA YAKE UVIMBE, BABA AKAMPACHIKA PEPO LA ULEVI

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye amejulikana kwa jina la Eriel Swai mkazi wa Ngaramtoni jijini hapa amekiri kumvika baba yake mzazi pepo la ulevi huku kwa upande wa mama yake mzazi  alimvisha tambara jeusi katika tumbo lake hali ambayo ilimfanya mama huyo kuwa na uvimbe mkubwa sana.

Akizungmza katika kanisa la uzima na ufufuo lilopo Maua Ungalmtd jijini hapa alisema kuwa aliamua kufanya hivyo kutokana na kuwa na nguvu za giza ambazo zilimuamuru kuwafanyia hivyo wazazi wake.

Kijana huyo alisema kuwa kwa zaidi ya miaka mitatu mfufulizo ameamua kuishi maisha ya nguvu za giza ambapo maisha hayo yalikuwa yakiwatumika hata wazazi wake bila ya wao wenyewe kujijua hali ambayo iliwasababisha waishi maisha ya mateso zaidi huku wakujua kuwa ni halali

Alibainisha kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfufulizo alilazimika kuishi katika maisha ya ufalme wa  nguvu za giza huku kivuli chake kikibaki duniani hali ambayo nayo iliweza kuwafanya watu wengi kujua kuwa ni yeye jambo ambalo lilikuwa si kweli.

“katika ufalme huo wa nguvu za giza mimi nilikuwa huko nikichimba makaburi lakini huku nyumbani ni kivuli ambacho kina sura ya mgomba ndicho kilichobaki pekee na wakati huo hicho kivulko killikuwa kikifanya mambo mbalimbali ambayo yalisababisha hasara kubwa sana”alisema kijana huyo.

Hataivyo alisema kuwa njia ambayo aliitumia yeye kama yeye kuenda katika ufalme huo wa nguvu za giza ni kupitia kwa bibi yake ambaye hapo awali alionekana kama amekufa lakini katika ufalme huo wa nguvu za giza hakuwa amekufa.

Naye Askofu wa kanisa hilo Bw Stanley kilima alisema kuwa kwa nyakati za sasa wazazi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawaweka watoto wao katika msingi wa imani kwa kuwa adui kwa sasa anawawinda sana watoto ambao ndilo taifa la Dunia

Alibainisha kuwa kama watoto watajali na kutoa kipaumbele zaidi katika msingi wa neon la Mungu ni wazi kuwa kamwe shetani hataweza kuwafanya wawe katika njia ambazo si sahihi ambazo ndizo chanzo pekee cha mateso ndani ya familia zao.

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891
ARUSHA 

No comments:

Post a Comment