Tuesday, February 28, 2012

NABII MALISA AWATAKA WAKRISTO KUTOA MAFUNGU YA KUMI, KUWA NA IMANI ILI KUONDOKANA NA UMASKINI

IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya watu ambao ni maskini wanashindwa kuinuka katika umaskini na kuingia kati hadhi ya utajiri kutokana na wao kujithaminisha sana na baadhi ya mali zao huku wakishindwa hata kumpa Mungu Fungu la Kumi

Umaskini uliopo kwa sasa ni fumbo kubwa sana baina ya watu na watu lakini chanzo kikubwa ni kutokuwa na maagano na mungu, pamoja na kushindwa kutoa mafungu ya kumi.

Hayo yameelezwa jijini hapa na Nabii Boniphace Malisa kutoka katika huduma ya Ukombozi ,Ministry for al Nationals wakati alipokuwa akiongea na wakristo wa mji wa Arusha mapema wiki hii.

Aidha Nabii Malisa alisema kuwa hakuna sehemu ambayo Mungu alisema wanadamu wawe maskini bali Mungu alisema kuwa  wanatakiwa kutawala vitu vyote vya duniani hali ambayo inaonesha wazi kuwa Mungu aliweka maagano .

Alisema kuwa katika nyakati za sasa asilimia kubwa ya watu wanalia kuwa wao ni maski ni bila kujua na kutambua kuwa umaskini walio nao wamejitakia wao wenyewe hata kwa njia ya kukiri na kukataa maagano na Mungu, pamoja na kutoa Mafungu ya kumi.

Alibainisha kuwa mkristo anapotoa Fungu la Kumi ni wazi kuwa anarudisha matoleo na sadaka ambazo amezipata kwa mungu lakini wanaoteswa na roho ya umaskini kwa sasa ni wale ambao hawana mambo mbalimbali kama vile Imani, Maagano ya kimungu, Mioyo ya kujitolea hali ambayo inatumika kama kigezo na Muovu shetani hasa pale mtu anapodai haki yake

“leo unakuta mtu anadai kuwa Mungu hamuonoi lakini ukiangalia hana hata agano lolote lile ambalo ameliweka yeye pamoja na Mungu sasa Mungu atasimamaje lakini mtu huyohuyo akienda kwa mganga anaweka agano na mganga Kwa Mungu inashindikana  je umaskini utaisha au utaongezeka mara dufu”alisema Nabii Malisa.

Pia amesema kuwa kanuni za maagano ya Mungu ni za msingi kwa mtu yoyote yule ambaye anataka utajiri kwa maana hiyo ni vema watu wakatafiuta maagano ya Kimungu na wala sio maagano ya Kidunia(ZABURI 50.5)

Katika hatua nyingine amewataka hata wale ambao wanaweka maagano dhidi ya Mungu kuhakikisha kuwa wanawajibika Vema na kukumbuka maagano hayo kwa kuwa hata katika jamii wapo baadhi ya watu ambao wanaweka maagano lakini wanashindwa kuyatekeleza.

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891
 ARUSHA 

No comments:

Post a Comment