Tuesday, February 28, 2012

WACHUNGAJI ARUSHA WALIA NA JESHI LA POLISI DHIDI YA MORANI
 
WACHUNGAJI wa kata ya Elerai mkoani hapa wamelitaka jeshi la polisi kuhakikisha kuwa wanachukulia sheria kali baadhi ya vijana wa kimasai”Morani”ambao wanawatembeza mitaani watu wakiwa utupu pamoja na kuwavisha magunia, na endapo kama jehi hilo halitaweza kufanya hivyo wao kama kanisa watafikiria mbinu nyingine ya kukabilana na Morani ambao wanawasumbua wananchi.
 
Akiongea na “NYAKATI” mapema leo kwa niaba ya wachungaji wa kata ya Elerai Sakina mchungaji Noel Urio alisema kwa muda mrefu sana vijana hao wamekuwa kikwazo kikubwa sana cha kufanya baadhi ya wakristoi kukosa amani.
 
Mchungaji Urio alibainisha kuwa Morani hao wamekuwa wakivamia makazi ya watu na kuchukua mali bila idhini na kisha kuwatembeza mitaani uchi huku wakiwa wamewavisha magunia huku jeshi la polisi likiwa na mbinu za kuweza kuwakamata Morani hao.
 
Waliongeza kuwa Jeshi la polisi ndilo lenye nafasi pekee ya kuweza kuwasaidia wananchi na kurudisha amani lakini mpaka sasa bado watuhumiwa hata wa sehemu nyingine hawajaweza kukamatwa na kutiwa mbaroni.
 
“hawa  Morani wamekuwa wakisumbua sana jamii kwa kuwa hata wale wa kipindi cha nyuma hawajatiwa mbaroni kwa maana hiyo sisi tunaomba ushirikiano dhidi ya hawa morani na kama hili litashindikana sisi tutajua kitu cha kufanya kama kanisa kwa kuwa na sisi wakristo tunahaki ya kuhakikisha kuwa tunaishi kwa amani”aliongeza Bw Urio.
 
Pia alisema kuwa Polisi pekee ndio wenye uwezo wa kuhakikisha kuwa wanatuliza gasia zote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanaishi kwa amani bila kufuata sheria au mila ambazo wanaona zipo kinyume na imani zao.
 
Alibanisha kuwa pamoja na Morani hao kutaka mila zifuatwe za Kimasai lakini kimsingi mia hizo zina madhara makubwa sana kwa kuwa hata njia ambazo zinatumika ni hatari sana kwa Afya.
 
Aliongeza kuwa Njia ambazo zinatumika katika kufanya tohara si njia njema kwa kuwa hata vifaa ambavyo vinatumika na vyenyewe havina ubora ambao unatakiwa kwa ajili ya afya ya mwanadamu hususani kwa nyakati hizi ambazo kuna maambukizi ya magonjwa mengi.
 
Naye mzee wa bomaBw Robert Elias  ambaye alitembezwa umbali mrefu yeye pamoja na mwanaye alisema kuwa katika siku ya tukio polisi walikuja lakini wakashindwa kumuokoa
 
Alilitaka Jeshi la polisi kuhakikisha kuwa wanawachukulia hatua kali na kisheria wale wote ambao wamehusika katika matukio hayo kwa kuwa mila ambazo Morani hao wanataka zifutwe tayari zimeshapitwa na wakati na ni hatari kwa afya ya Mwanadamu.
 
MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA 

No comments:

Post a Comment