Tuesday, February 28, 2012

MCHUNGAJI JOKA KUU ALIA NA MATAMBO YA MATAJIRI WA DUNIA

Matajiri mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuacha tabia ya kujisifu kutokana na mali zao na badala yake wahakikishe kuwa wanampa Mungu Utukufu kwa kuwapa mali, kwani baaadhi ya Matajiri, wenye Nguvu, na Hekima wamekuwa ni kikwazo kikubwa sana.


Katika jamii zetu wapo baadhi ya watu ambao wanajisifia sana kuhusuana na utajiri wao, hekima zao, na nguvu zao na kuona kuwa wao ni washindi katika maisha yao hali ambayo ni chukizo kubwa sana mbele za mungu.

Hayo yameelezwa na mchungaji Abati Joka kuu wa kanisa la MORIE  E.A.G.T lilopo katika maeneo ya Mbauda wakati akiongea na wauimini wa kanisa hilo mapema wiki hii.

Aidha Mchungaji Joka kuu alieleza kuwa kwa wale wenye tabia kama hizo wanatakiwa kuziacha kwa kuwa zinamkwaza sana Mungu na kwa hali hiyo inasababisha hata utukufu wa Mungu kushindwa kufanyika kwa wakati.

Aliongeza kuwa hao ambao wanatumia utajiri wao kwa kujisifia wanapata madhara mbalimbali katika maisha yao kwa kuwa Mkristo ambaye ana Mungu hashindwi na Jambo lolote wakati wale ambao wanajisifia mbele za Watu wanakosa hata maitaji yao

"Maandiko yanasema kuwa mwenye hekima asijifu, mwenye nguvu naye asijisifu kwa ajili ya hayo bali mimi ni bwana nitendaye wema, kwa maana hiyo tunapaswa kumpa Mungu peeke utukufu na wala sio Mali zetu"alisema Mchungaji Joka Kuu.

Alianisha kuwa pamoja na kuwa utajiri, nguvu, na hekima ni lazima ziwepo kwa Mwanadamu lakini wanadamu wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vitu hivyo kwa kumrudishia Mungu utukufu na wala sio kujisifia mbele za Macho ya wanadamu.

katika hatua nyingine mchungaji huyo aliwataka wakristo kuhakikisha kuwa wanamjua Mungu kwanza na mengine ya dunia nayo yatafuata kwa kuwa ndani ya jamii pia  wapo baadhi ya watu ambao wanajali zaidi Mali kuliko kumjali Mungu wao.

Alitaja madhara ambayo yanaweza kumkumba mtu ambaye anajali zaidi mali, pamoja na kujisfia kuwa ni pamoja na kukosa amani ya roho pamoja  na uhuru ambapo kwa wale ambao wanamtanguliza Mungu na kumpa Mungu utukufu juu ya mali zao wanaweza kupata amani ya kudumu.

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA 

No comments:

Post a Comment