Friday, April 5, 2013

ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI ZAIDI ACHANENI NA HABARI ZA SEMINA NA MIKUTANO- MWOLEKA


ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI ZAIDI ACHANENI NA HABARI ZA SEMINA NA MIKUTANO- MWOLEKA



Kushoto ni Malkia  wa  Matukio Arusha, na kulia ni Rose Jackson wakiwa wanatafakari jambo katika mtandao,hawa pia ni baadhi ya waandishi wa habari pia wakiwa kazini


Na Gladness Mushi,Arusha

WAANDISHI wa habari hapa Nchini wameaswa kuhakikisha kuwa wanajiwekea utatibu wa kuandika zaidi habari za uchunguzi kuliko kurtegemea habari za semina na mikutano kwani habari za mikutano na semina bado hazitoi majawabu na changamoto kwa jamii

Endapo kama waandishi wa habari wa Tanzania wataweza kujiwekea utaribu wa kuandika habari ambazo zina uchunguzi wa kutosha basi watakuwa ni chanzo kikubwa sana cha maendeleo ya Nchi

Hayo yalielezwa Jana na Anjelo Mwoleka ambaye ni Mkurugenzi wa Jambo  Arusha Publisher wakati  akiongea na wahitimu wa fani ya uandishi wa habari katika chuo cha uandishi wa habari Arusha (AJTC) katika maafali ya sita ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.

Aidha Mwoleka alisema kuwa kwa sasa kuna wimbi kubwa la waandishi wa habari a wanajihusisha zaidi na masuala ya habari za Semina na kuachana na habari za kiuchunguzi hali ambayo wakati mwingine ina nyima haki za msingi za jamii kwa kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa sana ya kuibua maovu yanaoendelea kwenye Jamii

Alifafanua kuwa habari za uchunguzi ndani ya Nchi ya Tanzania ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hivyo basi wana habari hawapswi kukimbia na badala yake wanapswa kuzipa kipaumbele kikubwa ili kuweza kuruhusu changamoto kwenye sekta zote kujilikana

“kuwa mwandishi wa habari sio lazima uwe unajua ratiba za mikutano za kila siku bali kuna maana kuwa unapaswa kujua na kutambua kuwa unatakiwa lkuwa mchunguzi na hapo ndio kazi yako itakuwa na manufaa makubwa sana kwa jamii hivyo basi habari za muhimu zinatakiwa kupewa kipaumbele tena kikubwa sana ili nchi ya Tanzania iweze kufika mahali ambapo inatakiwa kufika kama zilivyo nchi nyingine ambazo zimeendelea duniani”aliongeza Mwoleka


Awali wahitimu wa mafunzo hayo ya uandishi wa habari katika ngazi ya cheti, na shahada walisema kuwa pamoja na kuwa chuo hicho kimewalea katika maadili mazuri lakini bado wanakabiliwa na uhaba wa vifaa kama vile Kompyuta, na Kamera kwa ajili ya mazoezi.

No comments:

Post a Comment