Tuesday, April 9, 2013

ASKOFU SIXBERT ATANGAZA KURUDISHA AMANI YA ARUSHA


ASKOFU SIXBERT ATANGAZA KURUDISHA AMANI YA ARUSHA

Na Bety Alex,Arusha

KANISA  la Victorius Church  Hema ya Ukombozi  Sakina limetangaza kuwa kwa sasa ndani ya Mji wa Arusha hakutakuwa na maasi mbalimbali ikiwa ni  pamoja na vita ambavyo vinasababishwa na mambo mbalimbali na badala yake  historia mbaya ya mji wa Arusha itafutika na historia ya amani itaaanza kujiandika yenyewe

Akiongea na “nyakati”mara baada ya kuwekwa wakfu na kuzinduliwa kwa kanisa  na hema hilo jipya lililopo maeneo ya Sakina askofu wa kanisa hilo Sixbert Paul alisema kuwa ameingia rasmi ndani ya mji wa Arusha hivyo  ni lazima mabadiliko yaanze kuonekana

Askofu huyo alidai kuwa amepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge hivyo ni lazima mji uweze kurudisha heshima yake ambayo ulikuwa umepewa ikiwa ni  pamoja na kupunguza na kuondoa idadi ya maovu ambayo yanatokea zaidi katika mji wa Arusha

Alifafanua kuwa kupitia madhabahu yake ni lazima uponyaji tena wa hali ya juu sana uweze kutembea na pia uweze kuokoa watu ili lengo lake halisi liweze kufikiwa na faida za madhabahu yake ziweze kiutumika hata na viongozi wa kila aina huku hali hiyo pia ikichangia uwezo wa kumrudishia Mungu sifa na utukufu

“nimekuja Arusha rasmi sasa ni lazima kila roho ambayo iko kinyume na mapenzi ya Mungu iweze kusalimu amri na kuondoka nataka historia mpya kwenye maisha ya kila mtanzania wa Arusha.kwa hiyo watu waanze kujiandaa kwa  uponyaji na amani ya mkoa wa huu”aliongeza Askofu huyo

Pia alisema kuwa kupitia madhabahu yake ni Lazima hata hali ya maisha ya wakazi wa mji wa Arusha iweze kubadilika tena kwa kiwango cha hali ya juu sana na kila mtanzania kuwa na maisha yenye ubora na uhakika wa kiwango cha hali ya juu kwa kuwa madhabahu yake inatenda.

“kazi kubwa ya madhabahu hii ni kufungua watu katika shida na kisha kuwaweka huru hivyo kama watawekwa huru ni raisi sana kwao kuhakikisha kuwa wanakula mema ya nchi yaani maisha yao yawe na ubora wa hali ya juu na kuachana na maisha ya shida ambayo yana mwanzo na pia yana mwisho”alisema

Hataivyo wakristo mbalimbali ambao walihudhuria uzinduzi huo walisema kuwa wanaratarajia kuona mabadiliko makubwa sana ambayo yatasababishwa na hema hilo kwa kuwa hapo awali Arusha ilikuwa na Vita kubwa sana ya kisiasa hali ambayo ilipoteza maana halisi ya Arusha na hivyo kusababisha umaskini mkubwa kwa baadhi ya watu wakiwemo wafanyabiashara.

MWISHO

No comments:

Post a Comment