Tuesday, April 9, 2013

ASKOFU ALITAKA TAIFA LA TANZANIA KUTOJIBU VITA YA MASHAMBULIZI YA AINA YOYOTE ILE


ASKOFU ALITAKA TAIFA LA TANZANIA KUTOJIBU VITA YA MASHAMBULIZI YA AINA YOYOTE ILE

TAIFA la Tanzania pamoja na watu wake wameaswa kuachana  na tabia ya kulipizana kisasi cha aina yoyote ile badala yake lihakikishe kuwa linalipa ubaya kwa wema hali ambayo itaweza  kuwanyanya watanzania dhidi ya machafuko mbalimbali yanayoendelea ndani na nje.

Kauli hiyo imetolewa Mjini Arusha mapema jana na  askofu wa kanisa Katoliki Jimbo la Arusha,baba askofu Josephat Lobulu wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na maazimisho ya miaka 50 ya kanisa hilo yanayoendelea mjini hapa

Askofu huyo alisema kuwa kwa sasa Nchi ya Tanzania imekumbwa na machafuko mengi sana lakini si jambo jema kama wananchi au taifa litaachia amani  na kisha kuingia kwenye malumbano ambayo wakati mwingine yanasababisha maafa hata kwa wasio kuwa na hatia

Alifafanua kuwa kamwe jambo baya haliwezi kuisha kwenye jamii kama litalipzwa kwa ubaya bali jambo baya litaweza kuisha endapo kama litalipzwa zaidi kwa wema huku wema huo ukiwa ni viashiria vya amani ambayo wakati mwingine inapotea kutokana na ubaya ambao umo kwenye jamii

“kama nchi ya Tanzania tutataka kupoteza amani basi tuanze kuyafuta na kutafuta vyanzo vya vitu mbalimbali ambavyo vimezaa maovu ni wazi kuwa damu za watu wasiokuwa na hatia zitamwagika bure sasa mimi nawasihi sana watanzania wahakikishe kuwa wanalinda amani yao na wasiwe chanzo cha kuharibu amani ya taifa lao”aliongeza Askofu Lobulu

Akiongelea Sekta  za elimu na afya ambazo zimo chini ya kanisa hilo alisema kuwa mpaka sasa kanisa hilo hususani kwa mkoa wa Arusha limeshaweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa watanzania ambapo elimu hiyo pia itaweeza kupambana na adui Ujinga pamoja na adui Umaskini

Aliongeza kuwa kwa kuwa na sekta nzuri ya elimu ambayo itaweza kuwaruhusu watanzania kujipatia elimu pia kutaweza kuraisisha maisha ya vijana wa kitanzania ambapo kama watakuwa na elimu ya kutosha basi wataweza kukimbia hata maasi ya Taifa ambayo wakati mwingine yanatokea kwa kuwa hakuna kazi za kufanya


“tumedhamiria kuwa kwa sasa tunataka tuwe na elimu ya juu lakini pia hata kuweza kuiboresha zaidi ambapo itatoa fursa kwa vijana wengi zaidi lakini pia tutaweza kufikia malengo yetu ambayo tumejiwekea ya kutaka kuwafanya vijana wa kitanzania kuwa na elimu kama zilivyo nchi nyingine “alibainisha Askofu Lobulu

MWISHO

No comments:

Post a Comment