Friday, April 5, 2013

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAANZA MKAKATI WA KUFUA MITAMBO YA UMEME

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAANZA MKAKATI WA KUFUA MITAMBO YA UMEME






Chuo cha Ufundi Arusha kimeanza mkakati wa kufufua mitambo ya kuzalishia umeme wa maji wa Kituo cha Kikuletwa iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo hadi itakapokamilika itaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na umeme mwingine kubaki.

Ufafanuzi huo umetolewa na  mkuu wa Chuo hicho Dk Richard Masika kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama aliyetembelea mitambo hiyo ambayo imekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)

Alisema kuwa chuo hicho ambach kitakuwa cha kwanza barani Afrika kumiliki kituo cha kufua umeme,kitatumia kituo hicho kwa malengo matatu ambayo ameyataja kuwa ni pamoja na kutumika kwa mafunzo,kutengeneza vipuri vya mitambo ya umeme pamoja na kuzalisha umeme.

Dk Masika ameeleza kuwa baada ya kukabidhiwa kituo hicho mapema wiki iliyopita na baadaye kuanza kazi za awali wamebaini kwamba kwa kufunga mitambo mipya ya kufua umeme wataweza kutoa megawati 17 ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.



Alisema kuwa mitambo ya kituo hicho chenye eneo la jumla ya Ekari 400 yanategemea maji ya mito miwili ambayo Kware unaoanzia Mlima Kilimanjaro na Mto Mbuguni unaonzia mlima Meru ambapo maji hayo huduma katika kipindi kizima cha mwaka na kuongezeka wakati wa kiangazi

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanajro,Gama amewataka wataalamu wa cuo hicho pamoja na mipango mizuri na kuonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kukiendesha lakini aliwataka kuwa na uzalendo ambao utalisaidia taifa katika kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameahidi kukipa ushirikiano chuo hicho na kukitaka kuhakikisha kinaimarisha kitengo chake cha uhusiano ili kujenga mahusiano na vijiji vinavyozunguka kituo hicho.


Makunga alisema kuwa ni vyema chuo hicho kikajipanga kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya katika kuhakikisha kinawaelimisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani ili watambue umuhimu wa kituo hicho na madhara ya kutaka kuingiza mifugo kwa nguvu

No comments:

Post a Comment