Tuesday, April 29, 2014

SHULE YATOA UFADHILI WA MILIONI 90 KWA WANAFUNZI 90 KWA KILA MWAKA


SHULE YATOA UFADHILI WA MILIONI 90 KWA WANAFUNZI 90 KWA KILA MWAKA

SHULE ya Sekondari Edmund iliopo Sinon Mjini Arusha imetenga kiasi cha zaidi Milioni 90 kwa wanafunzi 90 kila mwaka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaotokea katika mazingira magumu huku lengo likiwa ni kuwaepusha na mimba za utotoni lakini pia uvunjifu wa amani kwenye jamii
hataivyo fedha hizo zinatolewa na wafadhili wa nje ya nchi pamoja na mfuko wa shule hiyo ujulikanao kama Mfuko wa Edmund ambao pia huo unalenga kuhamasisha ufadhili wa ndani
Hayo yameelezwa na Mkwabi Francis ambaye ni mkuu wa shule hiyo wakati akiongea na wanafunzi, wazazi pamoja na walezi wa shule hiyo kwenye maafali ya nane ambapo jumla ya wanafunzi 240 wanatarajia kuhitimu katika shule hiyo.
Mkwabi alisema kuwa mpango huo wa kuwasidia watoto wanaotokea katika mazingira magumu umeweza kuwanufaisha watoto wanaotokea katika vijiji vya Murieth, Mkono,Nadosoito,Ungalmtd, na Sinoni ambapo walengwa ni wale wenye maitaji muhimu
alifafanua kuwa walengwa hao ni wale watoto wanaotokea katika familia ambazo hazina uwezo,na mayatima ambapo watoto hao huweza kukupewa ufadhili maalumu kwa ajili ya kusoma na kupata elimu ya Sekondari.
"wafadhili wetu wakubwa wanatokea katika Nchi za Ausralia, Newzeland,Iland, na Marekani na hawa wanatufanikikishia hawa watoto 90 kuweza kupata elimu yao bora sana ya Sekondari ingawaje na sasa sisi tumejipanga kuhakikisha kuwa na sisi hapa hapa shuleni tunatoa ufadhili kwa watoto wetu ili siku hata kama tukikosa wafadhili basi tunaweza kusaidia jamii'aliongeza Mkwabi
Pia alisema kuwa nao wazazi wanapaswa kujua na kutambua kuwa nao wana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwasaidia watoto hasa wale ambao hawana uwezo wa kupata elimu ya sekondari kwani kupitia njia ya ufadhili wa ndani inawezekana kabisa
"kama wazazi, na walezi wakiwa na tabia ya kuchangia sekta ya maendeleo ya shule hasa mifuko ya shule  basi wataweza kusaidia jamii na hatutaweza kuwategemea zaidi wafadhili ambao wanatokea nje ya nchi kwani wakati mwingine wanapokatisha ufadhili wao wanasababisha watoto wawe kwenye hali ya uoga'aliongeza Mkwabi.
Wakati huo huo Wanafunzi wa shule hiyo ambao ni wahitimu waliwashauri walimu wa shule hiyo lakini pia wale wa shule nyingine kuachana na tabia ya kuwatenganisha wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha nne dhidi ya wale wa kidato cha tano na sita kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha wale wa vidato vya chini kutopata hamasa ya kujiunga au kufanya vema ili kuweza kujiunga na kidato cha tano na sita.
MWISHO

No comments:

Post a Comment