Tuesday, April 29, 2014

WAFANYABIASHARA WAPEWA MBINU YA MABOMU

NA MWANDISHI WETU, ARUSHA


jeshi la polisi mkoa wa Arusha limewaomba wafanyabiashara pamoja na wanachi wote ambao wanakuwa kwenye mikusanyiko mara kwa mara kuhakikisha kuwa wanatumia camera aina ya CCTV ili kuweza kujiepusha na majanga hasa ya mabomu.

Hataivyo kauli hiyo inakuja siku moja mara baada ya kutokea kwa mlipuko wa bomu ambalo linadhani kuwa ni bomu la kienyeji na kisha kulipuka katika baa moja ijulikanayo kama Arusha Night  Park
Kauli hiyo imetolewa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai Isaya  Mngulu wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya hatua ambazo wamezichukua mpaka sasa juu ya matukio hayo ya mabomu kwa mkoa wa Arusha.


Kamanda Isaya alisema kuwa watu wakichukua tahadhari basi wataweza kuwasaidia wengine kuepukana na vifo ambavyo sio vya lazima kwani kwa sasa magaidi wanaitesa sana jiji la Arusha.

Alidai kuwa kupitia camera hizo tahadhari inaweza kuchukuliwa tofautri na sasa ambapo kwa sasa asilimia kubwa ya mabomu ya kienyeji yanarushwa sana hasa kwenye mikusanyiko ya watu.


Hataivyo alishauri uongozi wa mkoa wa Arusha kuweka mikakati mbalimbali ya kuweka Camera hizo pande zote za Jiji kwani pia hilo nalo litaweeza kusaidia sana kupunguza uhalifu .


Kamanda Isaya alisema kuwa pamoja na kuwa wameweka mikakati mbalimbali ya kuweza kupunguza na kutokomeza uhalifu hasa wa mabomu katika maeneo ya mikusanyiko Polisi wanatarajia kufanya uchunguzi wa tukio hilo ambalo liliweza kujerui watu 15 ingawaje pia watatoa kitita cha Milioni 10 kwa mtu yeyote ambaye ataweza kutoa taarifa na kisha kufanikisha kukamtwa kwa mtuhumiwa.



Alimalizia kwa kusema kuwa katika tukio hilo la kurushwa kwa bomu la kienyeji katika nyumba hiyo ya kulala wageni hali za majerui zinaendelea vizuri na kwa sasa majerui nane wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Arusha.

Mbali na hayo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amewataka wananchi wa Jiji la Arusha wasiwe na hofu juu ya mikusanyiko ila wachukue tahadhari ingawaje kwa sasa wamejipanga kulinda ipasavyo hasa msimu huu wa majira ya sikukuu ya Pasaka.

sabas alidai kuwa wanatarajia kufanya ulinzi wa kutosha kwa kutumia vifaa mbalimbali kama vile Mbwa, Farasi, pamoja na Polisi wenyewe ili kuweza kuwafanya wananchi waweze kusherekea siku hiyo ya Pasaka.

MWISHO

No comments:

Post a Comment