Saturday, May 12, 2012

TANZANITE ONE YAIKUMBUKA WILAYA YA SIMANJIRO


TANZANITE Foundation ambayo ni kampuni tanzu ya TanzaniteOne ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara imechangia maendeleo ya jamii kwenye kijiji cha Naisinyai kwa kujenga shule mbili,zahanati,visima vya maji na kituo cha jamii.
 
Akizungumza wakati akigawa vifaa vya shule na michezo kwa wanafunzi wa shule ya msingi New Vision ya mji mdogo wa Mirerani,Mkurugenzi wa Tanzanite Foundation Hayley Henning alisema lengo lao ni kusaidia jamii na siyo kupata faida.
 
Henning aliongoza na wageni kutoka nchini Marekani wakiwemo waandishi wa habari Robert Weldan Weldo wa Gia na Steve Bennett wa Gems Tv alisema wapo kwa ajili ya kuimarisha na kudumisha imani na uadilifu wa Tanzanite.
 
Alisema walijenga baadhi ya madarasa ya shule ya msingi na sekondari Naisinyai,kliniki na visima vya maji kwa ajili ya kuboresha afya ya watoto wa eneo hilo walioathirika baada ya kutumia maji yenye floride nyingi.
 
“Tuliamua kuchimba visima hivyo baada ya watoto wengi wa Naisinyai meno yao kuwa na rangi ya hudhurungi hivyo hivi sasa maji hayo hayana tatizo hilo na wanatumia jamii pamoja na mifugo yao,” alisema Henning.

Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa American Gem Trade Association (AGTA) Doug Hucker alisema wamefurahia fursa ya kutembelea kampuni ya TanzaniteOne na kufahamu shughuli mbalimbali za madini ya Tanzanite zinazofanyika.
 
“Safari yetu baada ya maonyesho ya Arusha Internation Gem imetusaidia kuona hazina kubwa ya migodi ya Tanzanite na namna mnavyoijali jamii inayowazunguka kwa kuboresha hali ya maisha ya watoto wa Tanzania,” alisema Hucker.
 
Wageni hao walitembelea eneo hilo baada ya kutoka kwenye maonyesho ya kimataifa ya madini ya Arusha International Gem Fair yaliyofanyika wiki iliyopita na kuhusisha wafanyabiashara mbalimbali wa kimataifa.




0758907891

No comments:

Post a Comment