Monday, May 14, 2012

MADUKA 10 YAMEUNGUA KATIKA MJI WA NGARAMTONI



Maduka 10 yenye thamani ya zaidi ya million 100 yameteketea kwa moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni wilayaya Arusha vijijini ambapo chanzo halisi ni hitilafu ya Umeme

Akiongea na Majira katika eneo la Ngaramtoni  mmiliki wa maduka hayo Bw  Benjamini Mbayi alisema kuwa moto huo ulianza majaiara ya saa saba za mchana ambapo ulianza katika duka moja

Alisema kuwa wakati moto huo unaanza alilazimika kuingia kwenye chumba hicho na kuzima umeme katika kiunganisha cha umeme (SOCKET) lakini bado haikusaidia kabisa na moto huo uliendelea kutapakaa katikia vyumba bvingine vya biashara

“baada ya kuona moshi ukiwa unatapakaa kwenye paa ambapo  kwa kweli nilishindwa kuokoa kitu chochote ila nilifanya jitiada za kuhakikisha kuwa tunaomba msaada hasa kwa kikosi cha zima moto jambo ambalo lilifanikiwa ndani ya dakika 30”alisema Bw Mbayi

Pia aliongeza kuwa mara baada ya hapo kikosi hicho kilifanikiwa kuzima moto lakini vitu venye thamani ya Milioni 100 vilikuwa vimeshateketea kwa Moto lakini kutokana na zoezi hilo la uokoaji  hapakuwa na madhara yoyote yale ya kuunguwa kwa binadamu


Diwani wa kata ya Olmotony Bw David Kinisi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa kutokea kwa matukio hayo ya mara kwa mara ya moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni kunatokana na ubovu wa mundombinu hasa ya maeneo ya biashara hali ambayo kila mara inasababisha matatizo makubwa sana

Bw Kinisi alifafanua kuwa tukio la Moto katika mji huo wa Ngaramtoni ni la Pili ambapo mwezi uliopita  maduka tisa nayo yaliteketea kwa moto huku maduka hayo yakiwa na gharama ya milioni 200 huku moja ya maduka yakiwa ni mali yake


”kama mnavyoona hapa ubovu wa miundo mbinu unachangia kwa kiwango kikubwa sana na kama halmashauri haoitaweza kuliangalia suala hili kwa undani zaidi basi itakuwa ni hatari sana kwani kuuungua kwa maduka haya  ni dalili kubwa snaa ya umaskini hasa Ngaramtoni”alisema Bw Kinisi

Alifafanua kuwa hali hiyo inatakiwa kuboreshwa sana hasa katika eneo la Umeme kwa kuwa ndio  chanzo kikubwa Sana cha kutokea kwa majanga ya moto kwa kuwa hata maeneo yaliongua ndio chanzo kikubwa sana  cha hasara  na umaskini katika mji mdogo wa Ngaramtoni.

Awali aliwataka wananchi hasa wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanafanya biashara kwa kuzingatia utaalamu wa mafundi wa umeme na wala sio kwa kuwatumia mafundi wa uchochoroni ambao ndio chanzo kikubwa  cha majanga ya Moto

Naye kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa bado wanaendelea na  uchunguzi wa tukio hilo na kujua thamani halisi ya maduka yaliyoangua katika janga hilo
MWISHO


CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

No comments:

Post a Comment