Saturday, May 12, 2012

MAOMBI YASABABISHA KAKA MTU KUVUNJA PAA LA NYUMBA

MAOMBI YASABABISHA KAKA MTU KUVUNJA PAA LA NYUMBA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mke mmoja wa  muinjilisti wa makanisa ya Anglican Bi Elizabeth  Bakari amejikuta katika wakati mgumu sana mara baada ya kufanya maombi ya kuvunja malango ya kuzimu ambapo baada ya muda mfupi  kaka wa dada huyo alipoamua kuvunja  paa la nyumba yake kwa madai kuwa hamtambui

Akiongea na Nyakati mapema  wiki hii Bi Elizabeth alisema kuwa kilichofanya kaka yake ambaye anatambulika kwa majina ya Shabani Bakari ni malango ambayo yeye alikuwa akiyapinga wakati wa kuomba kwake

Alisema kuwa jumamosi iliyopita majira ya usiku alijikuta akiwa anapambana na maroho mbalimbali ambapo hali hiyo ilifanya kaka yake mzazi kutafuta ulimwengu mwingine na kisha kumshambulia ambapo pia hata zoezi hilo la kumnshambulia katika ulimwengu wa roho nao ulikwama

Alifafanua kuwa baada ya mapambano hayo ya muda mrefu sana  hayakuishia hapo na badala yake siku inayofuta ambayo ni jumapili iliyopita majira ya saa nne za asubui kaka huyo alivamia nyumba ya dada yake ambayo wanaishi na kisha kutoa mapaa kwa kisingizo kuwa hamtambui

“mimi nilishangaa sana kwa hali ya juu na kuona kuwa  ni jambo la ajabu sana kwa kuwa kaka yangu tena wa kuzaliwa nae anafanya vitu kama hivi lakini ninachojua ni kuwa  maombi ya vita niliyoyaomba ndio chanzo nah ii ni changamoto hata kwa wengine ambao wanafanya maombi ya kila siku hasa kwa maadui zao”alisema Bi Elizabeth

Alisema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo ambalo liliwavutia watu wengi sana ambapo baada ya muda alilazimika kwenda kwenye ofisi ya kijiji ili kupata haki yake ya msingi kwa kuwa kila mara baada ya maombi kaka huyo anamfanyia vituko vikali sana

Alifafanua kuwa mara baada ya kufika katika ofisi ya kijiji walimtaka afike kwenye kituo cha Polisi Kaloleni ili hatua za juu ziweze kuchukuliwa hali ambayo ilimfanya amtafute kaka yake chini ya uangalizi mkubwa sana wa jeshi la polisi

‘nililazimika kumtafuta chini ya jeshi la polisi kwa RB No KAL/RB/792/2012  ambapo alifanikiwa kukamatwa majira ya Jioni na kisha kuwekwa katika kituo kidogo cha Polisi ambapo  Jumatatu alifikishwa mahakamani na kujibu mashitaka ambayo yalikuwa yanamkabili

Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo kilichomfanya ampeleke katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso ili aweze kujifunza kwa undani wake kwa kuwa Neno msamaha limetakiwa kuwasemehe sasa kwa hali hiyo amemsamehe ili anachokitaka ni aweze kujifunza na anachokitaka ni maombi zaidi kwa kuwa inavyoonekana kaka yake ana matatizo makubwa hasa ya ulimwengu wa  roho

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA 

ARUSHA

0758907891

No comments:

Post a Comment