Saturday, May 12, 2012

KANISA LATAKIWA KUWAKUMBATIA ZAIDI VIJANA KATIKA MCHAKATO WA UJASIAMALI

MAKANISA mbalimbali hasa ya kanda ya kaskazini yametakiwa kuhakikisha kuwa yanasoma alama za nyakati kwa kuhakikisha yanasaidia sana vijana hasa katika mchakato wa ajira ambao unaanzia kwenye suala zima la Ujasiamali

Kwa sasa kama makanisa mengi yatahakikisha kuwa yanajiwekeza zaidi hata kwa kuhubiri na kuwapa moyo vijana walio wengi kuhusu umuhimu wa kuwa wajasiamali hata kama wameajiriwa basi watajiokoa kutoka matatizo mbalimbali zikiwemo anasa za dunia

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Mwenyekiti wa kanisa la Morovian jimbo la Kaskazini Tanzania,Mchungaji Peter Malema wakati alipokuwa akizundua kikundi cha wajasimali cha jijini hapa kijulikanacho kama SEMENS GROUP  wiki iliyopita

Mchungaji Malema alisema kuwa endapo  kama kanisa litasoma alama za nyakati na kuweza kujua hilo basi kwa kiwango kikubwa sana litakuwa limeweza kuwaokoa maelfu ya vijana ambao wengine wanateketea kwa kuwa hawana elimu hata ya ujasiamali

Aliongeza kuwa kwa muda huu ni vema kanisa likahakikisha kuwa linawaboreshea vijana bila kujali changamoto yopyote mafundisho hata ya ujasiamali ambayo yatalenga kuwaokoa na hivyo kama wataondokana na umaskini basi jamii nayo itakuwa imetua mzigo mkubwa

“kwa sasa ni vema kwa kila kijana wa kikristo kuhakikisha kuwa anakuwa mjasiamali kwa kuhakikisha kuwa anatafuta sana kwa kuwa hata maaandiko nayo yamewataka watafute na kama watafanya hivyo umaskini ndani ya nchi yetu utapungua kwa kiwango kikubwa sana”alisema mchungaji Malema

Awali mkurugenzi wa kampunin hiyo ya Semens Group  Bw Elias Semens alisema kuwa amejipanga kuhakikisha kuwa anawakomboa wakrisro hasa vijana na wanawake kwa kuwa wao ndio wenye mzigo mkubwa sana katika jamii

Alifafanua kuwa  kwa upande wa wanawake wanapopata elimu ya ujasiamali na kuwezeshwa kufanya kazi mbalimbali faida hiyo huenda kwenye jamii zao hali ambayo ni moja ya malengo ya makanisa mengi hasa kanisa la Morivian hapa nchini

Aliwataka viongozi wa makanisa mbalimbali kuhakikisha kuwa wanatumia kikiundi hicho ambacho kinahusika na usafi wa maofisini,na pia upishi kwenye halaiki kubwa ya watu ambapo hali hiyo nayo itaweza kuongeza hata chachu ya maendeleo ya kanisa na wajasiamali mbalimbali hapa nchini

MWISHO

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

No comments:

Post a Comment