Monday, May 14, 2012

MNAOTAKA ARDHI HAKIKISHENI KUWA INAKUWA NI KWA AJILI YA WAJANE NA YATIMA MERU

MBUNGE wa jimbo la arumeru mashariki Joshua Nasari amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwa na maono mbali mbali juu ya  matumizi bora  ya ardhi iliyopo wanayoitaka kutoka kwa wawekezaji  kwa kuhakikisha kuwa ardhi hiyo inajengwa vyuo vya ufundi na mambo mengineyo ambayo yatawasaidia wao  na vizazi vyao vijavyo

Nasari aliyasema hayo alipokuwa akiongea na wakazi wa jimbo hilo  katika hafla ya kumuaga muhasisis wa kanisa la African Mission Evangelism Askofu Nickson Issangya iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto yatima cha African Orphanag e kilichopo Sakila wilayani arumeru

Alisema kuwa pamoja na kuwa wana arumeru wanahitaji ardhi yao  kutoka kwa wawekezaji ,lakini  wanapaswa  wawe   na maono juu ya matumizi yake kwa kuwa wako ambao wakipewa ardhi hiyo  wanakimbilia kuuza ili wapate  fedha.

“Arumeru tuna matatizo mengi hatuna vyuo vya ufundi ,mji mdogo  ,wa usa river hauna hata viwanja vya kuzikia ndugu waliofariiki,hakuna hata viwanja vya michezo ila endapo mtakuwa na maono mazuri juu ya ardhi hiyo ni wazi kuwa  mtaifanyia mambo makubwa sana ya maendeleo”alisema Nasari

Aidha akielezea mikakati aliyonayo  alisema kuwa ni pamoja na kuhakikisha anawasaidia watoto yatima na wajane kwa kuwa makundi haya mawili yametekelezwa bila kukumbukwa  hivyo kuwafanya waonekane wametengwa na jamii.

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwasihi vijana kuachana na makundi ya kupotoshana na badala yake  wahakikishe wana kuwa na nidhamu ,maono . na uwajibikaji mzuri wa kazi kwa kuwa endapo watazingatia mambo hayo yatawafanya kufanikiwa katika maisha yao.

Nae mhasisisi huyo Nickson Issanya aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuweka itikadi za kisiasa pembeni na badala yake wawe na umoja kwa kuhakikisha kuwa wanampa mbunge wao ushirikiano ili aweze kutimiza malengo aliyojiwekea.

Issangya alisema kuwa endapo wataendeleza itikadi za kisiasa katika jimbo hilo ni wazi kuwa makundi hayatavunjika jambo ambalo litasababisha kurudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo.
mwisho



CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA


0758907891

No comments:

Post a Comment