Tuesday, May 27, 2014

UKOSEFU WA UPENDO KWA WALIMU CHANZO CHA UTORO MASHULENI

UKOSEFU WA UPENDO KWA WALIMU CHANZO CHA UTORO MASHULENI

Arusha


IMEELEZWA kuwa ili wanafunzi wa shule mbalimbali hapa nchini waweze kupenda shule na kuthamini masomo walimu wanatakiwa kuwa na lugha pamoja na malezi yenye upendo wa hali ya juu tofauti na sasa ambapo zipo baadhi ya shule ambazo zina walimu wasiokuwa na upendo.
Aidha kwa sasa wanafunzi wengi watoro wanakwepa shule kwa kuwa wamekosa matumaini ya upendo toka kwa walimu wao hivyo basi walimu wanapaswa kubadilika.
hayo yameelezwa na Kanali Mstaafu John Mongi wakati akizindua rasmi kamati ya bodi ya shule ya St Benedict Meliyo Primary  iliopo maeneo ya Sekei jijini hapa mapema jana.
kanali Mongi alisema kuwa neno upendo linapaswa kutumika sana ipasavyo na walimu, wakuu wa bodi pamoja na wazazi na kama litaweza kutumika ipasavyo basi litachangia sana hamasa ya elimu hapa nchini .

aliendelea kwa kusema kuwa kwa kukosa upendo kwa baadhi ya walimu kumekuwa chanzo kikubwa sana cha wanafunzi kuona shule kama ni uwanja wa vita na sababu hiyo hiyo pia imechangia sana hata utoro.
"tujifunze kwenye hizi shule ambazo zinaongoza kitaifa jinsi ambavyo walimu, bodi za shule zinavyowapenda wanafunzi,kwa hali hiyo basi mimi nasisiiza kuwa ili elimu iweze kufika katika kiwango cha juu lazima kwanza walimu wawe na upendo na wanafunzi ambao wanawafundisha"aliongeza Kanali Mongi.
hataivyo aliwataka nao walimu mbali na kuhamasiaha upendo  kwa wanafuzni ili kuweza kuepukana na majanga ya utoro shuleni lakini pia muda ambao wanakuwa na wanafunzi wao wahakikishe kuwa wanawaambia juu ya madhara yaliopo hapa nchini kama vile mdondoko wa maadili ili kuweza kuokoa kizazi cha vijana ambacho kwa sasa kinaangamia.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Joseph Laiser alisema kuwa ili kufanya elimu hapa nchini iweze kufikia katika kiwango ambacho kinaitajika tayari shule hiyo imeweka mikakati ya kuwapa semina wazazi , pamoja na viongozi mbalimbali wa shule hiyo .
Laiser alifafanua kuwa kwa kuwapa semina wazazi, walezi, na viongozi wa shule kutaweza kusaidia walengwa wa watoto hao kujua majukumu yao kwani kwa sasa shule nyingi zinashindwa kutekeleza majukumu yake kwa kuwa wanakwamishwa na vitu mbalimbali likiwemo suala zima la wazazi pamoja na walezi .
MWISHO

No comments:

Post a Comment