Tuesday, May 27, 2014

UROHO, UPENDELEO WA UTOAJI WA MISAADA KUTOKA KWA WAFADHILI CHANZO KIKUBWA CHA WAFADHILI KUTOKOMEA GIZANI



NaBety Alex, Arusha

IMEELEZWA kuwa Tabia ya uroho na upendeleo unaofanywa na baadhi ya
Viongozi wa Dini, Serikali na Jamii kwa ujumla kwenye ugawaji wa
misaada kutoka kwa wafadhili ndio chanzo kikubwa sana cha Watoto wenye
mahitaji muhimu kutelekezwa na wafadhili.

Hataivyo pia tabia hizo zimekuwa chanzo na kisingizo kikubwa sana cha
makundi maalumu kuweza kusahaulika na hivyo kujikuta wakiwa
wanakabiliwa na hali ngumu sana ya maisha ikiwemo ukosefu wa mahitaji
muhimu.

Hayo yameelezwa na Mchungaji Nakembetwa Shakademasi kutoka katika
kanisa la T A G Kindness Chrstian Centre(KCC)lilopo Ungalmtd wakati
akikabidhi msaada wa ngyo kwa watoto 50 wa eeno hilo la ungalmtd
mapema jana.

Shakademasi alisema kuwa tabia hiyo kwa sasa imejaa kwa viongozi ambao
wapo kwenye sekta mbalimbali hali ambayo inakimbiza  wafadhili wa
ndani na hata wa nje ya nchi.

Alifafanua kuwa, jamii haipaswi kuwa na uroho dhidi ya msaada wowote
ule unaelekezwa kwehnye kundi maalumu wakiwemo watoto bali jamii
inapaswa kuwaunga mkono wafadhili hata kama wametoa vitu ambavyo ni
vizuri kuliko vile vya familia ambazo zina uwezo.

“katika miaka ya sasa inashangaza sana wafadhili wanaogopa kutoa
msaada kwa jamii kwa kuhofia kuchakachuliwa wakati watoto hasa wale
ambao wanatokea mazingira magumu wanakabiliwa na changamoto lukuki za
kimaisha , tunapswa kuwa waminifu hata kama misaada ni mizuri kuliko
ile ambayo tunayo”aliongeza

Katika hatua nyingine alisema kuwa ili wafadhili waweze kuongezeka
hapa nchini misaada inatakiwa kuwafikia walengwa ambao wamekusudiwa
jambo ambalo litaweza kuokoa maisha ya watu walioko kwenye makunid
maalumu.

Pia Mgeni Rasmi kwenye  Hafla hiyo Mchungaji Peter Kitila alisema kuwa
nao watanzania wana uwezo mkubwa wa kuwa wafadhili wa ndani,na kuacha
kutegemea ufadhili kutoka nje ya nchi.

Kitila alidai kuwa kama kila mtanzania akijitolea kuwasaidia watu
wenye maitaji maalumu basi umaskini ndani ya nchi utaweza kupungua kwa
kiwango kikubwa sana tofauti na sasa ambapo wengi bado hawana hamasa
ya kusaidia makundi maalumu yaliopo kwenye jamii.

MWISHO

No comments:

Post a Comment