Thursday, May 29, 2014

ILBORU YADAI KILICHOSABABISHA MIGOMO YA WANAFUNZI MARA KWA MARA NI WANASIASA OVYO


UONGOZI wa Shule ya Sekondari Ilboru iliopo Jijini hapa umeweka utaratibu maalumu wa kuwakataa wanasisasa shuleni hapo kwani tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa wapo baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia kofia zao za siasa na kuwavuruga wanafunzi
Hataivyo miezi michache iliopo shule hiyo ilipata misukosuko kutokana na migomo mbalimbali ambayo ilifanywa na wanafunzi huku vichocheo vikubwa vikiwa ni wanasisasa wa Jiji la Arusha ambao walikuwa wanataka wanafunzi hao waingine kwenye mifumo ya vyama vya kisiasa.
Akiongea na Gazeti hili mapema jana mkuu wa shule hiyo ya Ilboru Julius Shulha alisema kuwa kuanzia sasa uongozi wa shule hiyo umeweka mikakati ya kuwakataa wanasiasa kuwatumia wanafunzi hao.
"unajua kuwa migogoro ambayo ilionekana shuleni hapani kutokana na wanasiasa na kuanzia sasa tumewakataa na hatutataka waje ili wawavuruge wanafunzi wetu tena"aliongeza Shulha
Alidai kuwa hata hao wanasiasa ambao wanatumia mwanya wao kwa ajili ya kuweza kuwayumbisha wanafunzi wanatakiwa waache mara moja kwani wanapaswa kujua nakutambua kuwa wao tayari wana mwanagaza wa maisha ila wanafunzi hao badi hawana mwangaza wa kimaisha.
"unakuta mwana siasa ana taaluma lakini anaajira yake tayari lakini anamuweka mwanafunzi huyu katika kundi lake na akifukuzwa hapa anaanza tena kutangatanga kwanini tusiwaache wanafunzi wakasoma alafu badae ndio wakajiingiza kwenye siasa lakini wakiwa tayari na elimu yao tunabdidi sisi watanzania kuanzia sasa tubadilike tuwaache wanafunzi wajisomee"aliongeza Shulha.
Kutokana na hali hiyo ya wanasiasa kuyumbisha shule hiyo alisema kuwa mpaka sasa wameshachukuatahadhari kubwa sana ya kuweza kuwasaidia wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na kuwaambia madhara ambayo yanaweza kujitokeza iwapo watajihusisha na siasa pindi wanapokuwa mashuleni
Alimalizia kwa kuwataka hata walimu wa shule nyingine nazo kuhakikisha kuwa wanapingana na siasa ambazo mpaka sasa zinaletwa mashuleni kwani hali hiyo ndiyo chanzo kikubwa sana cha wanafunzi kuingia kwenye migogoro na migomo ya kila siku.
MWISHO

No comments:

Post a Comment