Tuesday, August 27, 2013

MAASKOFU NA WASIMAMIZI WA MAKANISA FUATILIENI MAADILI YA WACHUNGAJI WENU ILI WASIWABISHE-ASKOFU MGONJA





IMEBAINIKA kuwa kutokana na tabia ya Maaskofu na wasimamizi mbalimbali wa makanisa kushindwa kuwafundisha wachungaji wao jinsi ya kuitumikia jamii ya kikristo ndio chanzo pekee cha baadhi ya viongozi wa dini kupata dharau ambazo haziwahusu.

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Askofu Aminiel Mgonja wa kanisa la Arusha Praise centre lilopo Sekei wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo juu ya maadalizi ya mahafali ya wachungaji 30 wa kanisa hilo yatakayofanyika mapema wiki ijayo

Askofu Mgonja alisema kuwa wasimamizi wa makanisa lakini pia maskofu wanatakiwa kuwa na utaratibu a kuwafundisha mambao mbalimbali wachungaji wao ili nao watakapofundisha waumini wawe na umoja na wala sio mgawanyiko

Alisema, kupitia mafundisho ambayo yatakuwa yanatolewa mara kwa mara juu ya wachungaji yartaweza kuwajenga kiimani lakini pia kiroho kwani asilimia kubwa ya wachungaji wa sasa wanakabiliwa na mambo mengi sana

Alibainisha kuwa watakapojijenga kiroho na kiimani kutaweza kuruhusu hata kazi ya bwana iweze kutendeka kwa wepesi zaidi kuliko pale ambapo kazi ya kulinda na kuwahifadhi kondoo itakapofanywa na wachungaji pekee yao.

“kama wachungaji wakiharibu kazi ya bwana basi sifa chafu haibaki kwao tu bali inabaki kwenye kanisa zima lakini pia inabaki kwa maaskofu sasa kabla hatujakubali kuchafiliwa ni lazima sisi kama maaskofu tujiwekee taratibu za kuwafunidhs kila mara hata kama wanaelimu ya uchungaji”aliongeza Askofu huyo

Wakati huo huo alidai kuwa hata nao wachungaji wa sasa wanatakiwa kuangalia zaidi msingi wa maandiko kuliko msingi wa mambo ya dunia ambayo wakati mwingine wanasababisha wawe wachungaji wa shetani

Alisema ni vema kama wakawa na tabia ya kufuata zaidi maadili na kuangalia ni aina ya huduma gani ambayo wanaitoa kwa mkristo kuliko kuacha maadili na kisha kujikuta wakiwa wameshazama ndani ya dhambi hivyo kusababisha madhara ya madharau ndani na hata nje ya kanisa

Kanisa hilo linataarajia kuwafanyia maafali wachungaji wake 30 ambao wamehitimu kozi na mafunzo ya uchungaji huku somo kubwa kwao likiwa ni maadili ya uchungaji kwa jamii yote hapa duniani

No comments:

Post a Comment