TANZANIA
INAKABILIWA NA MAFUNDI SANIFU MAABARA-MULUGO
TANZANIA inakabaliwa na tatizo la uhaba wa mafundi Sanifu Maabara ambapo kwa sasa
wanaozalishwa na Vyuo vya Ufundi hapa nchini hasa Arusha Techical College(ATC)ni
ndogo sana hali ambayo inafanya baadhi ya shule za Sekondari hapa nchini kukosa
ufanisi zaidi na Masomo ya Sayansi
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa elimu na Ufundi hapa
Nchini Bw Philiph Mulugo wakati akiongea na wadau mbalimbali wa chuo cha ufundi
Arusha(ATC)mapema wiki hii
Aidha Mulugo alisema kuwa bado hali si shwari hasa katika
sekta hiyo ya mafundi sanifu wa maabara kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi yenye
shule za Sekondari zaidi ya 400 wakati wanaozalishwa wakiwa bado ni 15
Alisema kuwa hali hiyo inasababisha kuwepo na uhitaji mkubwa
sana wa mafundi
sanifu kwa kuwa ili shule yoyote ile iweze kufanya vema katika masomo ya
Sayansi ni lazima kwanza wataalamu hao waweze kuandaa vifaa mbalimbali vya
maabara ili kuruhusu wanafunzi wasome vizuri
“hapa unaweza kuona kuwa wahitimu wa hii fani wachache sana kuliko wahitimu wa
darasa la saba ambao wanatarajia sasa rasmi kuanza rasmi masomo ya Sayansi sasa
kwa hali hii hata wale walimu wa masomo haya kwa kweli wanazidiwa sana na
majukumu lakini kama watakuwa na wataalamu wa kutosha tunaamini kabisa ufaulu wa masomo haya utaongezeka sana hivyo
Serikali itaondokana hata na uhaba wa
wataalamu mbalimbali”aliongeza Mulugo
Mulugo pia alisema kuwa pamoja na uhaba huo wa mafundi
sanifu wa maabara lakini lengo la Serikali la sasa ni kuhakikisha kuwa kila
shule inakuwa na Wataalamu hao ambao
wataweza kushirikiana na walimu wa Sayansi hivi karibuni ambapo pia hata Vyuo
vya ufundi navyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinajiwekea utaratibu wa kuzalisha
wataalamu wengi zaidi
Alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania kuhakikisha kuwa kamwe
hawakimbii fani hiyo badala yake wajiunge na Chuo hicho cha Ufundi Arusha ili waweze kudahiliwa kama wataalamu
ambapo hali hiyo itaweza kuokoa Jamii ambayo bado inakabiliwa na changamoto
ya uhaba wa wataalamu hao
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt Richard Masika
alisema kuwa kwa sasa Jamii inaona Masomo ya Sayansi ni Magumu kwa kuwa hakuna
utaratibu wa kuyafundisha kwa vitendo jambo ambalo kwa sasa chuo hicho
kimejipanga sana kuweza kujipanga kudahili wahitimu wengi zaidi ili kufanya
masomo hayo yasionekane ni magumu
Dkt Masika alisema kuwa ili masomo hayo yasionekane kuwa ni
magumu kwa sasa wamejiopanga kwa kuhakikisha kuwa wanazalisha wataalamu wengi
zaidi ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 watakuwa wamezalisha wataalamu zaidi ya
150 ambao wataweza kusaidia sana
kuokoa shule zenye uhaba wa watalaamu hao
MWISHO
No comments:
Post a Comment