Na Queen Lema,LONGIDO
WABUNGE WA MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUHUDHURIAVIKAO VYA ALAT ILI KUCHANGIA MAENDELEO YA MKOA
WABUNGE wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa
wanahudhuria kwenye vikao vya jumuiya za Serikali za mitaa(ALAT)na kuachana na
tabia ya kukwepa vikao hivyo kwa muda
mrefu sana kwani michango ya wabunge inaweza kuimarisha jumuiya hiyo pamoja na mkoa wa Arusha ambao unahitaji majibu
badala ya maswali kutoka kwa Viongozi.
Hayo yameelezwa jana wilayani Longidio na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Serikali za Mitaa kwa Tawi la Arusha(ALAT)Goodson Majola katika
kikao cha wadau wa Jumuiya hiyo na
Viongozi wake
Majola alisema kuwa wabunge wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanahudhuria
vikao kwa kuwa wanajua na kutambua shida na changamoto mbalimbali ambazo zimo
kwenye jamii lakini kama watakuwa hawahudhurii
vikao bado jamii itaendelea kuwa na changamoto mbalimbali
Aliongeza kuwa wabunge wanapokwepa vikao mbalimbali hasa vya
jumuiya za Serikali za Mitaa kunasababisha
maendeleo kuwa hafifu sana
kwenye jamii huku wannachi nao wakiwa na
hisia tofautitofauti juu ya utendaji kazi wa wabunge hao pamoja na Halmashauri
zao.
“sasa hivi wabunge wanatakiwa kujua na kutambua kuwa jamii
ambayo inaongoza haitaji maswali bali inahitaji majibu na hii pia ni hata ndani
ya halmashauri zetu kwa hiyo mpaka sasa wabunge wanatakiwa kutumia Jumuiya hii
na kushirikiana na kisha kutatua kero za jamii,lakini kama watakuwa wanakimbia
vikao ni wazi kuwa Jumuiya hii haitaweza kufikia malengo yake”aliongeza Majola.
Katika hatua Nyingine Katibu wa Jumuiya hiyo,Khalifa Idda
alisema kuwa endapo kama wadau mbalimbali pamoja na watalamu wa Halmashauri zaa
Mkoa wa Arusha wataweza kutumia Jumuiya hiyo vema basi wataweza kusaidia hata
Halmashauri kuepukana na Hati chafu ambazo zimekuwa zikisumbua sana baadhi ya halmashauri.
Idda alisema kuwa kupitia Jumuiya hiyo wataweza kujadili
mambo mbalimbali ambayo yanasababisha na kuwa kikwazo cha hati chafu hivyo
suala la hati chafu kutoka kwa mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG)litakuwa ni ndoto
hivyo kuongeza hata ufanisi zaidi wa kimapato.
“suala la hati chafu limekuwa kikwazo kikubwa sana kwenye
Halmashauri zetu lakini kama watu watakuwa na umoja na watashiriki kwa undani
sana kwenye ALAT basi wataepukana na hilo kwa kuwa hapa tutaweza kujadili kwa
wale waliofanikiwa kuvuka na hata wale walioshindwa na wenyewe tutaelezana kisa
kikubwa ni kipi hivyo ni vema kila halmashauri na wataalamu wake wakatumia vema
jumuiya hiyo”aliongeza Idda
MWISHO
No comments:
Post a Comment