WATOTO WA KIKE WAKIPEWA MOYO NA MOTISHA WANA UWEZO WA
KUSHIKA NAFASI ZA JUU KATIKA MITHIANI YA KITAIFA
,Arusha
IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya watoto wa kike wanashindwa
kufanya vema katika mithiani ya mwisho pamoja na masomo ya Sayansi kwa kuwa
wanakatishwa tamaa na jamii zao hasa walimu na wazazi
Watoto wa kike wana uwezo mkubwa sana
wa kufanya vema na kushika nafasi za juu katika masomo na mithiani yao lakini kwa sasa
wanakabiliwa na changamoto ya kukatishwa tamaa hali ambayo inawafanya washuke
Kitaaluma
Hayo yameelezwa na Mwanafunzi bora katika
Mthiani wa darasa la saba mkoa wa
Arusha, na Wilaya ya Arusha Vijijini,Pricilla Calvin Marealle wakati akiongea
na Majira mapema jana kuhusu kiwango cha Ufaulu wa watoto wa kike kwa mkoa wa
Arusha
Alisema kuwa watoto wa kike wana uwezo mkubwa sana wa kufanya vema katika mithiani yao
ya Mwisho na hivyo kushika nafasi ya juu Kitaifa endapo kama
mfumo ambao upo katika baadhi ya familia na Shule utabadilika
Akielelezea mfumo huo ambao unasababisha wanafunzi wa kike
kushindwa kufanya vema ni pamoja na kukatishwa tamaa hasa katika masomo ya
Sayansi na hivyo wanafunzi wa kike kuishia kuambiwa kuwa masomo ya Sayansi ni
masomo ya wanafunzi wa Kike hali ambayo nayo inachangia sana
wanafunzi kubweteka sana
Aliongeza kuwa mfumo mwingine mbaya ambao unasababisha kwa
kiwango cha juu sana wanafunzi wa kike kushindwa kufanya vema katika masomo yao
ni pamoja na wazazi, na walimu kukaa mbali na wanafunzi wao na hivyo kushindwa
kuwapa moyo wa kufaulu huku wazazi wakiona jukumu hilo ni kwa ajili ya walimu
na walimu wakiona kuwa jukumu hilo ni kwa ajili ya wazazi hali ambayo
inawafanya watoto wa kike kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea
“Mimi naweza kusema kuwa nimekuwa mtoto wa pili Kimkoa na wa
Kwanza kimkoa kwa kuwa walimu wangu na wazazi na ndugu zangu walikuwa
wanafuatilia maendeleo yangu tangu nilipokuwa madarasa ya awali na pale
nilipoanguka walitafuta chanzo na kunipa
moyo na motisha mbalimbali ndio maana niliweza kufika hapa na hivyo wazazi na
walezi wanatakiwa kujifunza juu ya suala hili kama wanataka wanafunzi waweze
kufaulu”alisema Pricilla
Awali alitoa wito kwa Serikali nayo kuhakikisha kuwa
wanaboresha zaidi shule za Kata hasa upande wa Maabara ambapo kwa sasa napo
kuna changamoto Lukuki ndani ya shule hizo hali ambayo inafanya hata wakati
mwingine wanafunzi wa shule za Kata kuonekana kama ni watoto wa maskini
kutokana na uhaba wa vifaa vya kujifunzia.
MWISHO
No comments:
Post a Comment