WILAYA YA ARUSHA VIJIJINI KWA KUSHIRIKIANA NA MBUNGE WAO KUANZA
RASMI MKAKATI WA KUJENGA HOSTELI SHULE ZOTE
Na Queen Lema,ARUSHA
Wilaya ya Arusha vijijini kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la
Arumeru Magharibi,inatarajia kufanya mabadiliko katika sekta ya elimu ambapo
kwa sasa wanatarajia kujenga na kuimarisha hosteli kwa ajili ya wanafunzi
hususani watoto wa kike ambao wanatembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta
elimu huku wakiwa mbioni kupatwa na Vishawishi mbalimbali.
Endapo kama tutajenga hosteli za kutosha basi hata kiwango
cha elimu yetu nacho kitaweza kupanda kwa hali ya juu sana tofauti na sasa ambapo wanafunzi
wanalazimika kupanga nyumba”GETO”ili wasome karibu na shule.
Hayo yameelezwa na Mbunge wa Arumeru Magharibi ambaye pia ni
Naibu waziri wa ardhi Goodlucky ole
Medeye wakati akikabidhi hundi kwa halmashauri ya Arusha vijijini ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari
Olokii mapema wiki hii.
Medeye alisema kuwa ameamua kuwa balozi wa hosteli kwenye
shule za Jimbo lake kwa kuwa bado watoto wa kike wanakabiliwa na changamoto
nyingi sana hasa ya kutembea umbali mrefu huku wengine wakipanga nyumba hali
ambayo inawafanya washindwe kusoma kwa raha huku hali hiyo nayo ikichangia sana
washindwe kufanya vema katika masomo yao.
Alisistiza kuwa lengo lake
halisi ni kuona kuwa hosteli zinakuwa
ni nyingi sana ambapo wanafunzi watakaa
mashuleni na kisha kusoma kwa raha huku pia hosteli hizo nazo zikichangia sana waweze kuondokana na
Vishawishi ambavyo wanakutana navyo wakati wakiwa njia kuja au kurudi majumbani
mwao
“Vishawishi kwa mtoto wa kike ni vingi sana lakini kama sote tutainuka na kuhaikisha kuwa hawa
tunakuwa na hosteli za kutosha basi itaweza kuraisisha sana maendeleo ya elimu
lakini kama tutakuwa na tabia ya kujivunia eti wingi wa shule wakati watoto
wanatembea umbali mrefu kutafuta elimu na barabarani wanakutana na vishawishi
kibao ni wazi kuwa bado tutakuwa hatujafanya chochote kipya kabisa”aliongeza
Medeye
Katika hatua nyingine alisema kuwa ili lengo hilo la ujenzi
wa hosteli liweze kukamilika tena kwa wakati katika baadhi ya shule ndani ya
Jimbo na Halmashauri yake ni lazima kuwepo na Ushirikiano tena wa hali ya juu
sana ili kuweza kuwanusuru watoto kutoka
katika nyumba za kupangisha”GETO”
MWISHO.
No comments:
Post a Comment