POLISI ARUSHA WAKUSANYA BILIONI 1.2 KUTOKANA NA MAKOSA
MBALIMBALI
Na Queen Lema,Arusha
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limefanikiwa kukusanya kiasi
cha Bilioni 1.2 kwa mwaka 2012 ambapo mwaka jana jeshi hilo
lilikusanya zaidi ya Milioni 518
kutokana na makosa mbalimbali ambayo yanatozwa mara baada ya wananchi
kuvunja sheria za Jeshi hilo
Akiongea na “MALKIA WA MATUKIO”jana kuhusuniana na mapato ya jeshi hilo
kwa mkoa wa Arusha kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kuwa
kuongezeka kwa fedha hizo kunatokana na jitiada mbalimbali za jeshi hilo za
kupambana na uhalifu.
Sabas alisema kuwa mbali na jeshi hilo
kuweza kupambana na uhalifu hivyo kukusanya kiwango kikubwa sana cha fedha lakini hata uhalifu wenyewe, ajali za
barabarani nazo zimepungua tofauti na
miaka ya nyuma kutokana na jitiada ambazo zinafanywa na Polisi
Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2011 matukio ya ajali
za barabarani yalikuwa ni 2507 wakati mwaka 2012 matukio yatokanayo na ajali
yalikuwa ni 2106 sawa na upungugu wa asilimia 16
Akiendelea kuelezea pia alisema kuwa hata matukio ya vifo vitokanavyo na ajali navyo
vimepungua kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo kwa mwaka 2011 matukio yalikuwa 211 huku 2012
yalikuwa ni 175 sawa na upungufu wa asilimia 17 ambapo hali hiyo imetokana na
Jitiada mbalimbali ambazo zinatokana na Jeshi hilo
Mbali na hayo pia makosa ya barabarani ambayo yamelipiwa nayo
yamechangia sana kuinua pato letu la mwaka ambapo yalikuwa ni zaidi ya elfu 42
kwa mwaka 2012 tofauti na mwaka 2011 ambapo makosa hayo yalikuwa ni 1978 sawa
na ongezeko la makosa ya barababarani yaliyolipiwa kwa asilimia 119
“Unaweza kuona matukio yamepungua kwa asilimia kubwa sana lakini pia hata mapato yetu nayo yameongezeka sana hivyo basi bado tunakabiliwa na changamoto ya
kuhakikisha kuwa masuala ya uvunjwaji wa sheria yanakwama kabisa ndani ya mkoa
wa Arusha kwani uwezekano upo na pia kama
tutafanya hivyo tutaongeza mapato lakini tutaokoa maisha ya Watu wa
Arusha”aliongeza Sabas
Kutokana na hali hiyo Kamanda Sabas aliwataka wananchi wa
Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanakuwa walindaji wazuri wa sheria za nchi na
wala sio wavunjaji wazuri wa sheria za Nchi kwani uvunjwaji wa sheria za nchi
ndio chanzo cha vifo ,Umaskini pamoja na Migogoro mikubwa sana ndani ya jamii.
MWISHO
No comments:
Post a Comment