LIPIENI MILIONI MBILI ZA ALAT TUTATUE CHANGAMOTO AMBAZO ZIPO
KWENYE JAMII ZENU KWA PAMOJA
Na Mwandishi wetu,ARUSHA
HALMASHAURI za mkoa
wa Arusha zimeagizwa kutoa kiasi cha Milioni mbili kama
mchango kwenye Jumuiya ya Serikali za mitaa kwa mkoa wa Arusha(ALAT)ambapo
michango hiyo itaweza kusadia na kutatua changamoto mbalimbali hasa kwenye
Serikali za Mitaa
Agizo hilo
limetolewa Mapema wiki hii na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Goodson Majola wakati
akiongea na wananchama wa umoja huo mjini hapa
Majola alisema kuwa ni vizuri kwa kila Halmashauri
kuhakikisha kuwa inachanga kiasi hicho na kuachana na tabia ya kukwepa michango
mbalimbalin kwani kwa kutotoa Michango ndani ya Umoja huo unachangia sana maendeleo kuwa hafifu sana
Alisema kuwa Michango hiyo ina umuhimu mkubwa sana hususani kwa wakati kama
huu ambao jamii inakabiliwa na matatizo
makubwa ambayo yanaitaji ufunguzi tena kuanzia ngazi za Serikali za mitaa.
“ni lazima kila halmashauri iweze kutoa na kuchangia kiasi
cha Milioni mbili kuanzia sasa na Halmashauri ambayo haitachangia kiasi hicho
kwa wakati kwa kweli hautaweza kuwatambua kwani chombo hiki kina nafasi kubwa
sana ya kuweza kutatua matatizo ya wananchi hivyo Umoja ni muhimu sana na
tutumie chombo hiki katika kutatua kero za wananchi’aliongeza Majola.
Katika hatua nyingine wadau wa Umoja huo walisema kuwa
pamoja na kuwa Halmashauri zinatakiwa kuachana na Tabia ya kukwepa Michango
mblimbali lakini Jumuiya hiyo inapswa kuhakikisha kuwa inatatua kero ambazo
zipo kwenye Serikali za mitaa hasa Migogoro ya ardhi na Mipaka.
Akiongea suala hilo Diwani wa Mwandeti,Boniface Tarakwa
alisema kuwa sehemu pekee ya kupata muafaka wa masuala ya migogoro ni kwenye
ALAT kwa kuwa ina meno ya kuweza kutoa
majibu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali hali ambayo itachangia sana
Amani.
Tarakwa aliongeza kuwa matatizo ya Migogoro ya Ardhi
imesababisha madhara makubwa sana
na inatakiwa kumalizwa tena kwa haraka kupitia kwenye umoja huo hasa kwa
kuyafikisha kwenye sehemu muafaka hasa kwenye vikao vikuu vya mkoa.
“Jambo la msingi hapa ni jumuiya hii ihakikishe kuwa
inamulika hata shida ambazo zipo na itusemehee kwenye ngazi za juu kwani zipo
baadhi ya ngazi ambazo zinatupiga chenga
na huku kwenye jamii tunaonekana kama wasanii hivyo Matumizi mazuri ya
jumuiya hii yatachangia sana
maendeleo na nafasi nzuri kwenye jamii ambayo tunaiongoza’aliongeza Tarakwa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment