Na bety alex,Arusha
MAASKOFU WATAKIWA KURUHUSU WALIMU KUFUNDISHA NYIMBO ZA
KUSIFU NA KUABUDU NDANI YA MAKANISA YAO
MAASKOFU wa makanisa mbalimbali ambao hawana uwezo wa
kutunga nyimbo mbalimbali za kusifu na kuabudu wametakiwa kuhakikisha kuwa
kamwe hawaachi makanisa yao
yakiendelea kupoteza uwepo huo bali wanatakiwa kuwatumia zaidi walimu ambao
wana uwezo wa kufundisha nyimbo za kusifu na kuabudu.
Kauli hiyo imetolewa na askofu Aminiel Mgonja wa kanisa la
Arusha Praise Centre la jijini hapa wakati akiongea na “MALKIA WA MATUKIO”mara baada ya
kutambulisha rasmi Album yake ijulikanayo kama
Ueponi mwako
Askofu Mgonja alisema kuwa kipajin cha kutunga kuimba nyimbo
za kusifu na kuabudu si watumishi wote ambao wana uwezo wa kufanya hivyo lakini
kutokana na kushindwa kufanya hivyo si sababu pekee ambayo itaweza kuyafanya
makanisa kushindwa kusifu na kuabudu
Alisema kuwa kama watumishi wa Mungu wataweza kuwapa fursa
baadhi ya walimu kuweza kufundisha na kutunga nyimbo mpya za kusifu na kuabudu
hali ambayo itawafanya Uwepo wa Mungu kuweza kusogea tena kwa haraka sana tofauti na sasa
ambapo baadhi ya makanisa yanashindwa kufungulia huduma hiyo.
Pia alisema kuwa hata kwa wale ambao wana uwezo wa kutunga
nyimbo za kusifu na kuabudu bado wana uwezo mkubwa sana wa kuendelea kuwa
wabunifu tena wa hali ya juu sana kwa
kuhakikisha kuwa nyimbo ambazo wanazitunga zinakuwa ni njia mojawapo ya
kuwasogeza watu uweponi mwa Bwana.
Katika hatua nyingine Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Album
hiyo ya Uweponi mwako,Askofu Olam Mustapha kutoka katika kanisa la
Gloryland,alisema kuwa mtumishi wa mungu anapofanya Jambo zuri hata watumishi
wengine nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafuraia jambo hilo na Kumuunga mkono na kuachana na tabia
ya kuchukiana ovyo
Olamu alisema kuwa wapo baadhi ya watumishi wa Mungu pamoja
na Wakristo ambao kila mara wanachukiana kwa ajili ya mafanikio ya Mtu lakini
hali hiyo ni mbaya sana
na ndio inayomtukuza shetani badala ya Mungu.
Pia katika uzinduzi huo wa Album hiyo zaidi ya Milioni tisa
zilikusanywa kutoka kwa watu mbalimbali huku
lengo halisi likiwa ni kumuunga mkono Askofu huyo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment