Na Queen Lema,Arusha
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mkuu wa Wilaya ya Arusha
John Mongela ameshukia Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Goodbless Lema mara baada ya mbunge huyo
kuifungia shule ya Sekondari Korona mapema jana na kudai kuwa mbunge huyon hana mamlaka ya kufunga shule
na asitumie kofia ya ubunge kuvunja Sheria na kuharibu amani ya Jiji la Arusha
Hatua hiyo imekuja leo mara baada ya Mbunge huyo
kufungia
shule ya sekondari Korona kwa madai kuwa shule hiyo bado changamoto
nyingi sana na hivyo wanafunzi wanasoma masaa mawili mpaka matatu hivyo
ni bora kila mwanafunzi ahamishwe na kwenda shule nyingine
Akiongea katika mkutano uliohitishwa na uongozi wa jiji la
Arusha Mkuu wa Wilaya,alisema kuwa,kitendo cha Mbunge Lema kufunga shule sio
kitendo cha kuvumiliwa kwa kuwa yeye
ndiye mtungaji wa Sheria lakini yeye pia ndiye mvunjaji mkubwa sana wa Sheria
hivyo pamoja na kuwa amefunga shule na kuwataka wanafunzi kuondoka ndani ya
shule hiyo bado hajawasaidia wanafunzi hao,kwa kuwa jumatatu asubui watarudi na kuendelea na masomo
Alifafanua kuwa endapo kama
Mbunge Lema angeona kuwa shule hiyo ya Korona ina matatizo ambayo ameyataja
basi angeyatatua kwa kuwa shule hiyo bado ipo ndani ya jimbo na pia ipo ndani
ya eneo ambalo anaishi hivyo bado anakuwa chanzo cha kudididimiza maendeleo ya
shule hiyo
“haiwezekani mtu akalale na mke wake nyumbani alafu kesho
aibuke aseme kuwa shule ya kata haina vigezo kama tutavumilia hili suala la
Lema basi kesho na diwani naye atafunga shule kwa kuwa haina vigezo na viwango
sasa mimi kama mkuu wa wilaya nasema kuwa hili suala halitavumilika
ingawaje pia baadhi ya madai ya Lema ni kweli ila kabla ya yote angetakiwa
aaangalie sheria ya mwaka 1995 inavyosema juu ya ufungaji wa shule”aliongeza
Mongela
Awali Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa madai ambayo Lema
ameyatoa ni ya kweli na pia anaungana nae ingawaje anachomlaumu ni kushindwa
kushirikiana na Viongozi ili Viongozi wazembe waweze kuwajibishwa kwa mujibu wa
sheria na taratibu za Nchi
Mongela alisema kuwa suala la ukosefu wa Maji,Vyoo, na Usafi
sio suala la hiari la kutekelezwa na Viongozi wa jiji bali ni suala la lazima
kutekelezwa ingawaje mpaka sasa changamoto kama hizo hazijatatuliwa kwenye
shule hiyo,na badala yake viongozi wa Jiji wamekaa ndani ya Ofisi zao ilihali
wanafunzi wanateseka sana
“Leo tunasema kuwa Lema amefunga shule lakini tuangalie
ukweli wa madai yake yupo sawa na mtanisamehe wakati mwingine mimi nitamuunga
mkono na kumsaidia katika mambo yake kwa kuwa
wapo baadhi ya watendaji wabovu
ndani ya Halmashauri mnashushia hadhi Serikali na kwa hili mtaondoka
mmoja baada ya mwingine na ninaanza na Mkuu wa Shule hii”alisema Mongela
“huyu mkuu wa shule ambaye ni John Ndewila amekuwa ni chanzo
kikubwa sana cha haya matatizo ambayo yamepelekea leo shule kutangaziwa
kufungwa sasa kwa hali hiyo nasema kuwa naanza nae kwa kumshusha cheo kuanzia
sasa ni mwalimu wa kawaida na mpaka jioni barua imfikie’aliongeza Mongela
Awali aliongeza kuwa wanafunzi wa shule hiyo wanatakiwa
kurudi shuleni hapo siku ya jumatatu na kuachana na kauli ya Mbunge kuwa shule
imefungwa lakini pamoja na hayo Jiji la Arusha kwa kushirikiana na
Mkurugenzi,na Afisa elimu sekondari wanatakiwa kuweka maji ndani ya siku moja
pamoja na kutatua changamoto za shule
hiyo lakini kama hawatafanya hivyo watavuliwa madaraka
Katika hatua nyingine Lema alisema kuwa kamwe Mkuu wa Wilaya
hapaswi kumuingilia katika majukumu yake kwa kuwa yeye amechaguliwa na wananchi
wakati Mkuu wa Wilaya ameteuliwa na Raisi
Lema alisema kuwa anachokitafuta machoni mwa watu na Mungu
ni haki na wala sio sifa kwa kuwa alipofunga shule hiyo alikuwa na viongozi wa
Serikali,kama Vile Afisa elimu Sekondari,Afisa utumishi na kwa hali hiyo ni vema kama Jiji
likasaidia na kutatua changamoto ambazo
zimo kwenye shule za Kata.
MWISHO
No comments:
Post a Comment