CCM MERU WATAKELEZA AHADI ZA CHADEMA
Na Queen Lema,Meru
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Meru(CCM) kimetekeleza ahadi
iliyotolewa na Viongozi wa Kitaifa wa chama cha demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA) kupitia kwa Mbunge wa jimbo hilo Joshua Nassari, ambapo
viongozi hao walitoa ahadi ya kuchimba Visima 11ndani ya siku 90 katika Kata ya
Maroroni kijiji cha Samaria lakini ahadi haijatekelezwa
Akiongea na Vyombo vya habari mapema jana Mwenyekiti wa Ccm
Wilaya ya Meru,Furaini Mungure alisema kuwa Viongozi wa Chadema ambao ni Dkt
Slaa,Ndesamburo, na Mbowe walitoa ahadi hizo wakati walipochukua jimbo la Meru
Mashariki lakini hawakutekeleza ahadi hiyo ambayo ikuwa inadai kuwa watapeleka
na kwenda kuchimba Visima 11 katika eneo Samaria Wilayani Meru
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo Ccm imeona kuwa kuna
umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa
wanatekeleza ahadi hiyo ambayo walikuwa wameahidiwa wananchi lakini bado
haijatekelezwa hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana
kutokana na ukame uliokithiri ndani ya maeneo hayo
Alifafanua kuwa pamoja na kuwa Viongozi hao wa Chadema
wametoa ahadi hiyo ya uchimbaji wa Visima lakini Ccm imeweza kufanikisha na
kutekeleza ilani yake ambayo inasema na kudai kutekeleza mahitaji mbalimbali ya
wananchi ambayo kama hayatatekelezwa
chanzo chake ni umaskini uliokithiri sana
“ahadi ilitolewa na Chadema na ilikuwa itekelezwe ndani ya
siku 90 mara baada ya Mbunge wao kupewa madaraka na wanananchi haikutekelezwa
lakini Sisi Ccm Tumetekeleza tena kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo shida
kubwa ya wananchi wa maeneo hayo ilikuwa ni uhaba wa maji sasa sisi kwa
kushririkiana na Halmashauri ya Meru
tumeweza kumaliza mchakato huo visima “aliongeza
Akielezea Utekelezaji wa Ahadi hiyo ya Visima 11 ambayo
ilitolewa na Chadema alisema kuwa Ccm tayari imeshakamilisha mchakato wa
kupeleka maji katika kijiji cha Samaria,
ambapo mpaka kufikia mwezi wa tatu wananchi hao watapata maji
Mungure alibainisha kuwa Chama chake kitajenga Tanki la maji
lenye ujazo wa lita elfu hamsini ambapo wananchi hao wataweza kupata maji kwa
uraisi sana tofauti na sasa ambapo wanalazimika
kutembea Umbali mrefu sana
kutafuta maji
Mbali na hayo alisema kuwa nao viongozi wa Ccm hawatakiwi kukaa maofisini
na badala yake wanatakiwa kwenda kwenye jamii na kuangalia jinsi ya kutatua
changamoto ambazo zinaikabili ili kuweza kutekeleza ilani ya Chama hicho.
MWISHO
No comments:
Post a Comment