Mbunge wa Jimbo la Longido Lekule Laizer amemtaka Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo kuhakikisha kuwa anatatua tena kwa haraka
migogoro ya kimipaka baina ya Wilaya na Wilaya kwani Migogoro hiyo imekuwa
ikichangia Umaskini mkubwa sana
Lekule aliyasema hayo wiki hii katika kikao cha Maendeleo ya
Mkoa wa Arusha (RCC) wakati akichangia hoja ya migogoro baina ya wilaya yake na
Wilaya za Arusha vijijini, pamoja na Monduli
Lekule alisema kuwa kwa sasa ni aibu kubwa sana
kuona Serikali ipo madarakani lakini suala zima la Migigogoro bado lishika
nafasi kubwa sana kwenye jamii hasa za wafugaji
na wafugaji hali ambayo nayo inaongeza
umaskini mkubwa sana
kwenye jamii hizo
Aliongeza kuwa Kamwe atakayeweza kutatua Migogoro hiyo ni
Mkuu wa Mkoa ambapo yeye kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali watatumia
elimu zao katika kusulihisha jambo ambalo mpaka sasa bado halijapatiwa ufumbuzi
tena wa Kutosha
“inanisikitisha sana kuona kuwa Mkuu wa Mkoa yupo lakini
bado migogoro ya ardhi ndio inashika kasi kubwa ndani ya jamii sasa tuende wapi
jamani na mbona hili ni jambo dogo sana
kwa mkuu wa Mkoa tunaomba sasa uamke na uje kuangalia suala hli la Migogoro kwa kweli linatuchosha sana”alisema
Lekule
Aliongeza kuwa kitu kikubwa sana
ambacho kitaweza kuepusha Wilaya za Arusha Vijijini,Monduli, na Longido katika
migogoro ya mipaka ni kuweka mipaka ambayo itaweza kuwaonesha wananchi ukomo wao baina ya sehemu
moja na sehemu nyingine hali ambayo nayo itaweza kurudisha amani na Umaskini
ambao umekithiri sana
kwenye jamii
“Kwa nini Mkoa unashindwa kuweka mipaka baina ya Wilaya na
Wilaya na ni kitu kidogo sana ambacho hakiitaji
Taaaluma kubwa sana sasa kwa kuwa hakuna mipaka
wananchi wengi sana
wanapigana kila mmoja akidai mwenzake kaingilia sehemu ya mwingine je tunalinda
amani au tunabomoa amani ya Nchi jamani ni lazima Mkoa lazima uangalie hili
suala la migogoro ya mipaka”alisema Lekule
Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo,alisema
,kuwa kamwe viongozi hawapaswi kuja juu kuhusiana na suala hilo la Migogoro ya
Mipaka bali wanatakiwa kukuaa na wananchi pamoja na wataalamu ili kutafuta
suluhu ya amani ambayo imepotea
Mulongo alisema kuwa suala hilo la Migogoro ya mipaka
watahakikisha kuwa wanalishugulikia tena kwa haraka sana lakini pia ili liweze
kufanikiwa kwa haraka sana ni lazima juhudi viongozi mbalimbali wa Wilaya
ziwepo ili kuondoa Tatizo hilo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment