Wednesday, January 16, 2013

SHIRIKA LABUNI MBINU MPYA YA KUWAFUATILIA MAMA WAJAWAZITO KWA SIMU ILI KUPUNGUZA VIFO NYAKATI ZA KUJIFUNGUA


SHIRIKA LABUNI MBINU MPYA YA KUWAFUATILIA MAMA WAJAWAZITO KWA SIMU ILI KUPUNGUZA VIFO NYAKATI ZA KUJIFUNGUA

 Jane Edward, ARUSHA

SHIRIKA  la Jhpiego  la jijini Dar es saalam limefanikiwa kubuni aina mpya ya mradi ujulikao kama Maisha ambapo mradi huo utaweza kutumia simu za mkononi kwa ajili ya kufuatilia afya za mama wajawazito  kwa malengo ya kupunguza vifo vya wajawazito

Akiongea na “malkia wa matukio”mjini hapa mapema leo Meneja mradi wa shirika hilo Dkt Dunstan Bishanga alisema kuwa mradi huo wa maisha umeanza kutekelezwa kwa mkoa wa Morogoro

Dkt Bishanga aliongeza kuwa mradi huo una malengo ya kuhakikisha kuwa inapunguza vifo vya mama wajawazito hapa nnchini lakini njia pekee ya kuwakutanisha wahudumu wa afya pamoja na wajawazito ni simu za mkononi hasa  kwa kuwapa wajawazito taarifa mbalimbali


Pia alisema kuwa Mradi huo ambao kwa sasa umeanza kutumika katika Mkoa wa Morogoro lakini wanaendelea kufanya tathimini mbalimbali za kuhakikisha kuwa unasambaa nchi nzima kwani una uwezo mkubwa sana wa kuokoa maisha ya mama wajawazito

Hataivyo aliongeza kuwa mara baada ya mkoa wa Morogoro kunufaika na mradi huo wataweza kwenda mikoani ikiwa ni pamoja na kuongeza zaidi ubunifu zaidi ili kuimarisha zaidi afya ya mama kwa manufaa ya Nchi nzima kwani vifo hivyo vinasababisha sana Umaskini katika jamii.

Awali alisema kuwa suala la mama wajawazito ni suala ambalo linatakiwa kuchukuliwa tahadhari kubwa sana ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu sahihi za afya kutoka kwa wataalamu hivyo nao wazazi wa kiume wana nafasi kubwa sana ya kufanya hivyo

MWISHO

No comments:

Post a Comment