FRANK LEONARD AKABIDHIWA MIKOBA YA MAREHEMU MWANGOSI IPC
mwenyekiti mteule wa IPC Frank Leonard (kushoto) na katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin kulia tukiteta jambo katika moja kati ya vikao vyetu mwaka jana |
Aliyekuwa mweka hazina wa IPC marehemu Vicky Macha |
Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Marehemu Daud Mwangosi na chini siku alipouwawa kinyama |
KLABU
ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) imekamilisha
kuziba mapengo ya uongozi yaliyokuwepo ndani ya IPC kufuatia kifo
cha
aliyekuwa mwenyekiti wake marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa tarehe
2/9/2012 Nyololo katika vurugu za polisi na Chadema kwa kumchangua
Frank Leonard kuwa mwenyekiti mpya wa klabu hiyo huku Francis
Godwin akiwa katibu mkuu wa IPC.
Mbali
ya kuziba nafasi hiyo ya mwenyekiti kwa Leonard aliyekuwa katibu
mtendaji kuamua kugombea uenyekiti na Godwi aliyekuwa katibu msaidizi
kugombea ukatibu mkuu pia wajumbe wa mkutano huo wame mchagua Janeth
Matondo kushika nafasi ya
mweka hazima mkuu wa IPC nafasi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa
mwekahazina Vicky Macha aliyefariki mwezi mmoja baada ya kifo cha
Mwangosi .
katika mkutano huo maalum wa uchaguzi huo uliofanyika leo katika Hotel ya M.R mjini Iringa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Frederick Siwale aliwataja waliochaguliwa kuwa ni pamoja na aliyekuwa katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard aliyepata kura 17 kati ya kura 18 zilizopigwa katika nafasi hiyo ya uenyekiti iliyokuwa ikigombewa na mwanachama Zulfa Shomari aliyetangaza kujitoa na kuomba wajumbe kumchagua Leonard kutokana na utendaji wake mzuri .

Wengine waliochaguliwa ni pamoja na mweka hazina mkuu wa IPC Janeth Matondo aliyechukua nafasi ya marehemu Vicky Macha kwa kupata kura zote za ndio 18 pamoja na mweka hazina msaidizi Suleiman Boki aliyepata kura zote 18 .
Wajumbe watatu wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni Hapy Matanji aliyepata kura (18) Swiga Mwaisumbe (18 ) na Selina Ilunga(17).
No comments:
Post a Comment