Na Queen Lema,Meru
TEKELEZENI AHADI MLIZOZITOA WAKATI WA KUOMBA KURA-OLE
NANGOLE
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha(CCM)bw
Onesmo ole Nangole amewataka Viongozi mbalimbali wa chama hasa wale ambao
walitoa ahadi kwa wananchi kwenye
uombaji wa kura kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi hizo kwa haraka sana kwani
wale ambao hawatekelezi ahadi wanachangia sana chama hicho kuelekezewa lawama
Bw Nangole aliyasema hayo Juzi wakati akifungua Kata mpya ya
Chama hicho ambayo kwa sasa inajulikana kama
Kata ya Majengo iliopo Meru Mkoani Arusha.
Aidha Bw Nangole alisema kuwa tabia ya baadhi ya Viongozi ya
kuwa watoa ahadi hasa nyakati za kura na kisha wakishapata kura wanasahau ahadi
zao inachangia sana
kuunguza Ccm kwenye jamii na kuonekana kuwa ni watoaji ahadi zisizotekelezwa.
Alisema kuwa Viongozi wote ambao walitoa ahadi mbalimbali
kwa wananchi hasa katika Nyakati za Kura
wanatakiwa kuhakikisha kuwa watekeleza ahadi zao na kujijengea tabia ya
kuwaangalia wapiga kura wao ili kuendelea kulinda uhai wa Chama
‘msihaidi tu wakati wa kura sasa anzeni kutatua kero za
wananchi pamoja na ahadi zenu kwa lkufanya hivyo mtakuwa mmetoa fursa kubwa
sana kwa chama chetu lakini kama mtakuwa mnahaidi na kisha kuingia Mitini huku
wananchi wakiwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hapo mtakuwa mmewapa
Vyama vya Upinzani nafasi ya kuongea”aliongeza Bw Nangole
Mbali na hayo aliongeza kuwa Viongozi mbalimbali wa Chama
hicho wanatakiwa kuangalia zaidi ilani ya chama hicho kwa kuhakikisha kuwa
wanaainisha matatizo ambayo yapo kwenye jamii na kisha kuyatatua kuanzia kwenye
Ngazi za Vitongoji na Vijiji.
“Suala la Maendeleo sio suala la kuanzia ngazi za juu za
uongozi bali ni suala la kuanzia ngazi za chini hata ninyi viongozi wa chini
mnatakiwa kuangalia Kero ambazo zinaikabili jamii na mtasaidia sana ingawaje kwa sasa wapo viongozi wa chini
kabisa ambao bado nao hawajitambui katika mchakato wa kuwasaidia wananchi”aliongeza
Bw Nangole
Katika hatua nyingine Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Meru
Bw Langaeli Akyoo alisema kuwa bado Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ambazo zinatakiwa zitatuliwe kwa haraka sana
ingawaje umoja na ushirikiano unaitajika kwa haraka sana
Bw Akyoo alisema kuwa kama Viongozi wa Chama hicho kwa
Kushirikiana na wananchi wataweza kuwa kitu kimoja basi watachangia sana Maendeleo na hata
mara nyingine kutimiza ahadi mbalimbali ambazo zilihaidiwa na chama hicho
lakini hazikutekelezwa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment