UGONJWA WA MAHINDI KUTOKA KENYA WAWAATHIRI WANANCHI KATA YA
KIKWE MERU
ZAIDI ya Hekari 300 kutoka katika kata ya Kikwe Wilayani
Meru mkoania Arusha zimeharibiwa vibaya na ugonjwa mahindi kutoka Nchini Kenya unaojulikana kama
ugonjwa wa kusinyaa kwa mahindi hali ambayo itafanya wakulima washindwe kupata
mahindi wakati wa mavuno
Akiongea na “patapata”mapema jana diwani wa kata hiyo bw
Emanuel Silayo alisema kuwa hali hiyo ya ugonjwa ambayo imekumba kata hiyo ya
Kikwe inaashiria njaa kubwa sana
kwa kuwa mazao ya mahindi shambani hakuna huku wakulima wakiwa wameshapanda
Silayo alisema kuwa Miezi michache iliyopita wakulima
waliweza kupanda mazao ya nafaka hasa mahindi lakini baada ya mahindi kuchomoza
yalianza kushambuliwa na ugonjwa hadi kufa
Alisema kuwa pamoja na kuwa mahindi hayo yamekufa wakati
wakulimna wengi wamepanda kwa ajili ya mategemeo ya chakula katika eneo hilo la Kikwe lakini mahindi machache sana
yameweza kusalia hali ambayo bado ni kiashirio kikubwa sana cha Njaa
Alifafanua kuwa kama tahadhari haitaweza kuchukuliwa kwa
haraka sana
basi huenda wakati wa mavuno ndani ya mwaka huu kusiwe na mavuno kabisa hivyo
baa la njaa kuweza kutawala katika Wilaya hiyo ya Meru.
Akiongelea Ugonjwa huo wa mahindi kutoka nchini Kenya Afisa
Kilimo Wilaya ya Meru,Grace Solomoni alisema kuwa ugonjwa huo ni hatari sana kwa kuwa unashambulia
zao la mahindi hadi kufa lakini bado mkulima anaweza kupata angalau kiasi
kidogo
Grace alisema kuwa kwa mujibu wa taararibui za kilimo mara
baada ya shamba kuathiriwa na ugonjwa huo shamba linapswa kupumzishwa kwa
kipindi cha miaka mitatu ili vijidudu vife lakini kama wakulima wataendelea
kulima basi watasababisha vijidudu hivyo
kuzaliana kwa wingi sana
No comments:
Post a Comment