MERU WAPATA HASARA YA MILIONI 30
KUTOKANA NA WAWEKEZAJI KUKIMBILIA KWENYE MPANGO WA EPZ
Na Queen Lema,MERU
HALMASHAURI ya Meru Mkoani Arusha
imepata hasara ya zaidi milioni 30 kwa kipindi cha miaka miwili mara baada ya
kukosa kodi katika mashamba makubwa mawili yaliopo ndani ya halmashauri ambapo
mashamba hayo yameingia katika mpango rasmi wa maendeleo ya uchumi na
viwanda(EPZ)
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri Trasias Kagenzi wakati akiongea na Baraza la Madiwani wa
Halmashauri hiyo katika kikao cha kupitisha bajeti ya Halmashauri hiyo mapema
jana.
Kagenzi alisema kuwa
Halmashauri hiyo imepata hasara ya ukosefu wa kodi kutoka kwa wawekezaji
wawili ambao wameingia katika mpango huo wa EPZ ambao walikuwa wanachangia kodi
kwa kiasi cha Milioni kumi na tano kwa mwaka.
Aliongeza kuwa
Wawekezaji wa mashamba hayo ambao wamehamia katika mpango huo ni
pamoja na Doll Esatate, huku Mwekezaji mwingine akiwa ni Delka Bruine ambapo
walikuwa wanchangia kiwango kikubwa sana cha kodi hali ambayo imesababisha
mapungufu makubwa sana.
Alisema kuwa hasara hiyo ya
Mamilioni ya fedha inachangia sana Halmashauri hiyo kushindwa kufikia malengo
yake mbalimbali ambayo wamejiwekea lakini pia mpaka sasa wameshabuni chanzo
mbadala ambacho kitaweza kufuta kwa kiwango hasara hiyo kubwa ambayo imetokana
na wawekezaji kujiunga na mpango wa EPZ
“hapo awali tulikuwa tunachukua
kiasi cha Milioni 15 kwa wawekezaji hawa wawili lakini kwa miaka miwili
tumekosa kodi zao kwa kweli hii ni hasara kubwa sana nah ii pia tutaitumia kama
changamoto hata kwa hawa wengine ambao nao wanampango wa kujiunga na EPZ kwani
kama tusipokuwa wajanja na tukabuni aina mpya ya vyanzo vya mapato basi
halmashauri itakuwa katika hali tete”aliongeza Kagenzi
Katika hatua nyingine alisema kuwa
mbali na kukosa Milioni 30 kama kodi lakini mpango huo utaweza kuwanufaisha
watu wengi hususani Vijana ambapo kwa awali utatoa ajira kwa Vijana zaidi ya
5000 huku hali hiyo ikichangia kwa kiwango kikubwa sana hata Ukuaji wa
Uchumi wa Meru
Kagenzi alifafanua kuwa wananchi wa
Meru wanatakiwa kutumia vema fursa ambazo zipo na wahakikishe kuwa kupitia
fursa hizo na wao wanakuwa wabunifu kwa kuweza kujiandaa hata kuanzia
sasa kuboresha bidhaa ili ziweze kuendana na soko la Nchi jirani
MWISHO
No comments:
Post a Comment