LEMA ATETA NA MAFISADI WANAOTUMIA MAKANISA NA MISIKITI KWA
AJILI YA KUJISAFISHIA
Na Queen Lema,ARUSHA
MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema ameyataka
makanisa na Misikiti hapa nchini kuachana na tabia ya kuwakumbatia mafisadi
kutokana na wingi wa sadaka zao na badala yake kuwaombea mafisadi hao waweze
kubadilika
Asilimia kubwa ya mafisadi bila kujali imani zao sasa
wanatumia sana Makanisa na Misikiti ili kwenda
kujisafisha kwenye jamii kwa kuchangia kiwango kikubwa sana cha fedha huku fedha hizo za sadaka
zikiwa ni fedha chafu
Lema aliyasema hayo Jijini hapa wakati akihutubia katika
mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo lake mapema
jana,huku lengo halisi likiwa ni kukumbuka siku ya January tano ambayo baadhi
ya wananchama wa Chadema walipoteza Maisha
Aidha Lema alisema kuwa tabia hiyo ambayo kwa sasa
imeibuliwa na mafisadi ya kujisafisha kupitia vyombo vya dini si tabia njema
kabisa bali ni tabia ambayo inapeleka nchi na kizazi chake mahala pabaya sana huku pia hali hiyo ikichangia Umaskini mkubwa sana kwenye jamii ya
watanzania
Alisema kuwa wananchi kamwe hawapaswi kukubaliana na hali
hiyo ya mafisadi sasa kutumia majumba ya ibada na kujisafisha bali na wao
wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya kazi ili waepukane na fedha chafu ambazo
zinatolewa na mafisadi kwenye majumba ya ibada kama
harambee
‘mimi nashangaa sana ninyi viongozi wa majumba ya ibada
ambao kila kukicha mnakaa na kuomba Rehema lakini Mafisadi wakija na Fedha
chafu hamuwaulizi na badala yake ndio mnawawekea mikono ya baraka sasa hamuwezi
kuona kuwa mnawawekea mikono waendelee na kazi yao ya kuwaibia wananchi wa
Tanzania?alisema Lema
Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kuwa yeye ni
Mbunge lakini kamwe hatukubali kuona kuwa anahujumiwa ili awaache wananchi wa
jimbo la Arusha mjini kwa kuwa wananchi hao ndio waliomuamini na wakampa kura
ili aweze kuwaongoza tena kwa njia ya uhalali kabisa
Alisisitiza kwa wananchi kuwa ipo haja ya watu wote kumrudia
zaidi Mungu na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa mwaminiufu kwani
uaminifu pekee ndio utakaoleta maendeleo ya Mkoa wa Arusha pamoja na Nchi ya Tanzania
tofauti na kutegemea fedha chafu za harambee kutoka kwa Mafisadi
Hataivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa
Arusha(CHADEMA)kiliweza kutoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu vya watoto
yatima huku lengo likiwa ni kukumbuka mauji dhidi ya wanachama wa chama hicho
yaliyofanyika January 5 mwaka jana.
MWISHO
No comments:
Post a Comment