Na Queen Lema,Arusha
TUTABORESHA HUDUMA ZA UGANI ILI
KUENDELEZA KILIMO KWANZA-MKURUGENZI ARUSHA VIJIJINI
HALMASHAURI ya Arusha Vijijini imesema kuwa itaendelea kuboresha huduma za
ugani ili kupitia wataalamu hao wa Ugani waweze kutatua changamoto mbalimbali
ambazo bado zinaikabili sekta ya Kilimo kwanza.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa wilaya hiyo Bw khalifa Idda
wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na Maendeleo,mikakati na
Changamoto mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo mapema juzi.
Bw Idda alisema kuwa Halmashauri yake imeamua kuendelea
kuboresha huduma za Ugani ambapo kupitia uboreshaji huo utaweza kuruhusu
mabadiliko makubwa sana
kwenye sekta ya Kilimo kwa kuwa Kilimo kinachangia Pato la Halmashauri hiyo.
Alifafanua kuwa bado zipo changamoto Lukuki ambazo
zinaikabili Sekta ya Kilimo lakini kama
wataalamu ambao ni maafisa Ugani watakuwa na Mazingira mazuri ya kufanyia kazi
basi wataweza kuruhusu mabadiliko makubwa kwani watatumia taalumu zao kwa
kuwasaidia wananchi.
“tumeamua kwanza kabla ya kuimba wimbo wa kilimo kwanza,tuwaangalie
hawa watendaji wakuu ambao ni maafisa ugani,ambapo tulikaa chini na kuona kuwa
kama watafanikiwa kupata mahitaji ya msingi basi wataboresha ujuzi wao katika
kutoa huduma za msingi kwa wakulima na wafugaji’aliongeza Bw Idda
Pia alisema kuwa,pamoja na kuendelea kuboresha mikakati
mbalimbali ya kilimo kwanza ndani ya Halmashauri hiyo lakini bado Sekta ya
Kilimo kwanza inakabiliwa na changamoto kubwa sana hali ambayo inafanya Halmashauri hiyo
kubuni njia mbalimbali za kuokoa kilimo kwanza.
Alisema kuwa Changamoto hizo ni kama
matumizi mabaya ya teknolojia duni katika shuguli za kilimo hasa jembe la
mkono,kilimo kisichozingatia hifadhi ya ardhi na maji,pamoja mabadiliko ya hali
ya hewa ambayo inaenda sanjari kabisa na ukame.
Katika hatua nyingine
alisema kuwa Changamoto hizo zimekuwa zikichangia mazao pamoja na mifugo kuwa
hafifu sana ingawaje Halmashauri hiyo inaendelea
kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa hali kama
hiyo ya kilimo hafifu inakuwa ni historia kupitia kwa mafias Ugani.
MWISHO
No comments:
Post a Comment