ARUSHA KUZINDUA KAMPENI YA USAFI FEBRUARY MOS,ATAKAYECHAFUA MAZINGIRA KUFIKISHWA MAHAKAMANI
Na Queen Lema,Arusha
Uongozi wa Jiji la Arusha kwa kushirikiana na kamati ya
usafi wa Jiji linatarajia kuzindua Kampeni ya usafi wa jiji ambapo kampeni hiyo
itaenda sanjari na utozwaji wa faini kwa wachafuzi wa mazingira
Akiongea na Vyombo vya habari mapema leo mwenyekiti wa
kamati ya mazingira Jiji la Arusha,Adolph Ulomi alisema kuwa uzinduzi huo
utafanyika FebruaryMosi na utashirikisha wananchi wote
Aidha Ulomi alisema kuwa Umoja ambao umeundwa baina ya jiji
na kamati hiyo utaweza kuwasaidia kusafisha Jiji la Arusha ambapo kwa sasa kuna
changamoto kubwa sana
ya uchafuzi wa mazingira
Alisema kuwa kupitia Kamati hiyo ya usafi wa mazingira
ambayo inaanza kampeni zake February Mosi itaweza kuhamiashisha shuguli
mbalimbali za usafi sanjari na kutoa,kuratibu,vifaa mbalimbali vya usafi
ambavyo hapo awali havikuwepo
‘Tumeamua kufanya mji wa Arusha kuwa na mabadiliko ya hali
ya juu sana
ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hadhi ya jiji inarudi mahala pake hivyo February
Mosi tutaanza kazi rasmi ndani ya jiji na tunatarajia kampeni hizi zizinduliwe
rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha”alisema Ulomi
Katika hatua nyingine alisema kuwa kupitia kamati hiyo ya
usafi wa Jiji la Arusha pia wataweza kusimamia sheria na kanuni mbalimbali za usafi ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kuwa wanaovunja sheria za usafi wanafikishwa mahakamani pamoja na
kutozwa faini kubwa
Aliongeza kuwa baadhi ya makosa ambayo yataweza kutiliwa
mkazo mkubwa hasa ya usafi wa jiji ni pamoja na kutema mate, kukojoa ovyo ndani
ya jiji,kutupa taka ovyo,pamoja na kufanya biashara ndani ya maeneo yasiyo
rasmi ambapo wakosaji wote watafikishwa mahakamani.
“unaweza kuona Abiria wanatoka mikoani lakini wanapoingia
ndani ya Mji wa Moshi wanaambiwa sasa unaingia Moshi hivyo wasitupe taka lakini
wanapoingia katika mji wa Arusha wanaambiwa kabisa wapo huru kuchafua hili tunataka liwe ni historia kabisa kwani
uwezo wa kufanya jiji liwe katika hadhi yake upo kabisa”aliongeza Ulomi
Pia alibainisha kuwa Kampeni hiyo ya usafi pia itaweza
kwenda sanjari na utoaji wa elimu ya mazingira ndani ya Mitaa zaidi ya 100
ambapo wananchi wataelezewa madhara ya uharibifu wa mazingira.
MWISHO
No comments:
Post a Comment