MFANYAKAZI
wa kampuni ya uwekezaji ya Tanzanite One inayochimba madini eneo la Mirerani,
wilayani Simanjiro, Willy Mushi (), ameuawa kwa kupigwa risasi na watu
wanaoaminika kuwa ni wachimbaji wadogo baada ya kukutana mgodini chini ya ardhi.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo alilosema
lilitokea Saa 6:00 usiku wa kuamkia jana na tayari ametuma timu ya upelelezi
unaoongozswa na Afisa upelelezi wa mkoa huo, kuchunguza zaidi tukio hilo.
Marehemu
alipigwa risasi mbili kufuani upande wa kushoto alipoongozana na mfanyakazi
mwenzake Kennedy Masimbaji kukikagua eneo la mgodi unaoingiliana na migodi ya
wachimaji wadogo.
“Tulipofika
kwenye mitobozano ambako kumepangwa mifuko ya viroba vya mchanga kutenganisha
mgodi wetu na ile ya wachimbaji wadogo, ghafla tukashambuliwa kwa risasi ambazo
zote zilimuingia marehemu kifuani na kufariki papo hapo,” alisema Masimbaji
Mfanyakazi
mwingine wa Tanzanite One, leonard Paul alisema tukio hilo ni muendelezo wa
mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na wachimbaji wadogo dhidi ya wafanyakazi wa
mwekezaji pindi wanapokutana chini ya ardhi ambapo siku kadhaa zilizopita
uongozi ulilazimika kusimamisha kazi kutoa fursa ya polisi kuchunguzi migogoro
ya mitobozano.
“Serikali lazima sasa ichukue hatua kuzuia matumizi
ya silaha za moto chini ya migodi,” alisema Paul
Kwa mujibu
wa Mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Tumsifu Mushi, marehemu ameacha
mjane na watoto wanne na taratibu za mazishi zinaendelea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment